Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili (interview) TANAPA August, 2024

Majina Ya Walioitwa Kwenye Usaili (interview) TANAPA August, 2024 PDF, Waliochaguliwa Usaili Leo tunayo taarifa muhimu kutoka kwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Kwa wale ambao waliomba kazi, usaili umefika. Ifuatayo ni maelezo muhimu mnayopaswa kuzingatia.

Tarehe na Muda wa Usaili

Usaili utaanza tarehe 03-08-2024 na kuendelea hadi 14-08-2024. Kila kada ina muda na sehemu maalum ya kufanyia usaili, hivyo hakikisha unajua ratiba yako.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia

Barakoa: Hakikisha unafika kwenye eneo la usaili ukiwa umevaa barakoa.

Kitambulisho: Kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni kama Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji.

Vyeti Halisi: Kuwa na vyeti vyako halisi kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea.

Gharama: Utajigharamia chakula, usafiri na malazi.

Vitu Vingine Muhimu

  • Wasailiwa walio na Testimonials, Provisional Results, Statement of results, na hati za matokeo za kidato cha IV na VI hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
  • Hakikisha unazingatia tarehe, muda na mahali ulipopangiwa kufanyia usaili.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NACTE au NECTA.
  • Waombaji ambao majina yao hayakuonekana kwenye tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi zitakapotangazwa.

Kada Maalum

Kwa kada zinazohitaji usajili na bodi za kitaaluma, hakikisha unakuja na vyeti vyako halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.

Hatua za Mwisho

  • Wale wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwani namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.

Walioitwa Kwenye Usaili (interview) TANAPA August, 2024 PDF

Hapa; https://www.ajira.go.tz/baseattachments/interviewattachments/

Kwa maelezo zaidi na ratiba kamili, tembelea tovuti rasmi ya TANAPA au Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Tunawatakia kila la heri katika usaili na maandalizi yenu. Kumbuka, nidhamu na maandalizi mazuri ndiyo funguo za mafanikio.

Soma Zaidi: