Nafasi Za Kazi MDAS Na LGAS 2024 Ajira Mpya (6,257)

Nafasi Za Kazi Mdas Na Lgas 2024 Ajira Mpya (6,257) pdf,  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara zinazo jitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs), anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi elfu sita, mia mbili hamsini na saba (6,257) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.


Nafasi za Kazi Zinazotangazwa

1. Msaidizi wa Ufugaji Nyuki Daraja la II (Beekeeping Assistant II) – Nafasi 47

Maelezo ya Kazi: Msaidizi wa Ufugaji Nyuki atahusika na kusimamia manzuki na hifadhi za nyuki, kukusanya takwimu za ufugaji nyuki, kutunza kumbukumbu za utafiti, na kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo. Atatoa leseni za biashara za mazao ya nyuki, ushauri wa kitaalam kwa wananchi kuhusu ufugaji endelevu wa nyuki, na kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.

Sifa za Mwombaji: Astashahada ya Ufugaji Nyuki kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, Kidato cha Nne au Sita.

Ngazi ya Mshahara: TGS B

2. Mpima Ardhi Daraja la II (Land Surveyor II) – Nafasi 4

Maelezo ya Kazi: Mpima Ardhi atahusika na kuingiza taarifa za upimaji kwenye kompyuta, kukagua kazi za upimaji, kufanya upimaji picha, kusimamia na kuchukua vipimo vya “tide gauges,” na kupima ardhi katika serikali za mitaa.

Sifa za Mwombaji: Stashahada ya Juu/Shahada katika Upimaji Ardhi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS E

3. Afisa Ununuzi Daraja la II (Procurement Officer II) – Nafasi 350

Maelezo ya Kazi: Afisa Ununuzi atashiriki katika kuandaa nyaraka za zabuni, kusambaza hati za zabuni, kuwasiliana na idara kuhusu mahitaji ya ununuzi, kukusanya taarifa ya bei za soko, na kuhakiki hati za madai kabla ya malipo.

Sifa za Mwombaji: Shahada/Stashahada ya Juu ya Ununuzi au Ugavi, au “Professional level III” inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

Ngazi ya Mshahara: TGS D

4. Afisa Uvuvi Daraja la II (Fisheries Officer II) – Nafasi 90

Maelezo ya Kazi: Afisa Uvuvi atasimamia uhifadhi wa rasilimali za uvuvi, kubuni mbinu za kudhibiti uvuvi haramu, kuratibu kazi za doria za uvuvi, na kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uvuvi bora.

Sifa za Mwombaji: Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Uvuvi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS D

5. Dereva Daraja la II (Driver II) – Nafasi 514

Maelezo ya Kazi: Dereva atahusika na kukagua gari kabla na baada ya safari, kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi, kufanya matengenezo madogo ya gari, na kujaza taarifa za safari kwenye daftari.

Sifa za Mwombaji: Cheti cha Kidato cha Nne, leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji magari, na mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari kutoka VETA au NIT.

Ngazi ya Mshahara: TGS B

6. Afisa Wanyamapori Daraja la II (Game Officer II) – Nafasi 26

Maelezo ya Kazi: Afisa Wanyamapori atatekeleza kazi za ushirikishaji wadau katika uhifadhi, kudhibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara, na kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya wanyamapori.

Sifa za Mwombaji: Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS D

7. Afisa Misitu Daraja la II (Forest Officer II) – Nafasi 91

Maelezo ya Kazi: Afisa Misitu atasimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu, kufanya utafiti wa misitu, kutekeleza sera na sheria za misitu, na kutoa ushauri kwa wananchi juu ya uendelezaji wa misitu.

Sifa za Mwombaji: Shahada/Stashahada ya Juu ya Misitu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS D

8. Afisa Mazingira Daraja la II (Environmental Officer II) – Nafasi 119

Maelezo ya Kazi: Afisa Mazingira atakusanya takwimu na taarifa za usimamizi wa mazingira, kutoa elimu ya hifadhi ya mazingira, kushiriki katika tafiti, na kufuatilia utekelezaji wa sera na sheria za mazingira.

Sifa za Mwombaji: Shahada ya kwanza yenye mwelekeo wa Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira katika fani kama Geography and Environmental Studies, Environmental Science and Management, n.k.

Ngazi ya Mshahara: TGS D

9. Afisa Usafirishaji Daraja la II (Transport Officer II) – Nafasi 56

Maelezo ya Kazi: Afisa Usafirishaji atatayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri, kuhakikisha kumbukumbu za vyombo vya usafiri zinatunzwa vyema, kukusanya takwimu za usafirishaji, na kutekeleza majukumu mengine yanayohusu sekta ya usafirishaji.

Sifa za Mwombaji: Shahada/Stashahada ya Juu ya Usafirishaji kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS D

10. Afisa Utalii Daraja la II (Tourism Officer II) – Nafasi 27

Maelezo ya Kazi: Afisa Utalii atakusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii, kutoa leseni za utalii, kukusanya takwimu za watalii, kupanga nafasi za masomo ya utalii, na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wadau wa utalii.

Sifa za Mwombaji: Shahada/Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani za Utalii au Hoteli kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS D

11. Afisa Ushirika Daraja la II (Cooperative Officer Grade II) – Nafasi 27

Maelezo ya Kazi: Afisa Ushirika atakagua vyama vya ushirika, kutoa elimu kwa wanachama, kufuatilia utekelezaji wa sheria na kanuni za ushirika, na kushiriki katika kutatua migogoro ya ushirika.

Sifa za Mwombaji: Shahada ya Ushirika au fani inayohusiana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Ngazi ya Mshahara: TGS D


Jinsi ya Kuomba: Waombaji wote wanatakiwa kuwasilisha barua za maombi, wasifu (CV), nakala za vyeti vya elimu na mafunzo, pamoja na nakala za vyeti vya kuzaliwa. Maombi yote yaelekezwe kwa:

Katibu, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
S.L.P. 63100,
Dar es Salaam, Tanzania.

PDF Hapa; https://www.ajira.go.tz/baseattachments/advertisementattachments/

Soma Zaidi: