Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania 2024/2025, Tangazo La Kuripoti Shule Ya Polisi Moshi Kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania Majina Yote,
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anapenda kutoa taarifa kwa vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi. Tafadhali zingatieni maelekezo yafuatayo kwa ukamilifu.
Tarehe za Kuripoti
- Kuanzia: 30/09/2024
- Mwisho: 02/10/2024
- Mahali: Shule ya Polisi Moshi
Vijana wa Dar es Salaam na Vikosi vya Makao Makuu
Kwa wale waliofanyiwa usaili Dar es Salaam (DPA) na Vikosi vya Polisi vya Makao Makuu:
- Mahali: Polisi Barracks, Barabara ya Kilwa, karibu na Hospitali Kuu ya Polisi
- Tarehe: 30/09/2024
- Muda: Saa 12:00 asubuhi
- Lengo: Safari ya kuelekea Shule ya Polisi Moshi
Vijana wa Mikoa ya Tanzania Bara
Kwa waliofanyiwa usaili katika mikoa ya Tanzania Bara:
- Mahali: Ofisi za Makamanda wa Polisi wa Mikoa
- Tarehe: 29/09/2024
- Muda: Saa 2:00 asubuhi
- Lengo: Kupata utaratibu wa safari kuelekea Shule ya Polisi Moshi
Vijana wa Zanzibar (Unguja na Pemba)
Kwa vijana waliofanyiwa usaili Zanzibar:
- Mahali: Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani)
- Tarehe: 29/09/2024
- Lengo: Kupangiwa utaratibu wa safari kuelekea Shule ya Polisi Moshi
1. Mavazi ya Michezo:
- Track suit bluu yenye ufito mweupe
- Fulana nyeupe isiyo na maandishi
- Raba na soksi nyeusi
- Bukta mbili za bluu (kwa ajili ya mazoezi)
2. Vifaa vya Malazi:
- Sanduku la chuma rangi ya bluu
- Chandarua cheupe cha duara
- Shuka za light blue (jozi mbili)
- Blanket moja la kijivu (sio duveti)
- Pasi ya mkaa
3. Vifaa vya Usafi:
- Reki
- Jembe lenye mpini
- Panga
- Ndoo mbili ndogo
- Fagio la chelewa
4. Nyaraka Muhimu:
- Kadi ya bima ya afya (NHIF) au Tsh 50,400 kwa wasio na bima
- Vyeti halisi vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, na kadi ya NIDA au namba za NIDA
- Passport size 6 (background blue)
- Nakala za vyeti (copy 5 kwa kila cheti kilichotajwa)
5. Fedha za Kujikimu:
Hakikisha una fedha za matumizi binafsi wakati wa mafunzo.
Tahadhari: Simu za Mkononi
- Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni. Ukipatikana na simu, utaondolewa mafunzoni mara moja kwa utovu wa nidhamu.
- Utaratibu wa mawasiliano utaelekezwa shuleni.
Mwisho wa Kuripoti
- Mwanafunzi yeyote atakayechelewa kuripoti baada ya 02/10/2024 hatapokelewa na atachukuliwa kuwa amejiondoa kwenye mafunzo.
Orodha ya Vijana Waliochaguliwa
Orodha kamili ya majina ya waliochaguliwa imeambatanishwa kwenye tangazo hili. TANGAZO-LA-KURIPOTI-SHULE-YA-POLISI-MOSHI.pdf
Imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Makao Makuu ya Polisi, Dodoma
23/09/2024
Usikose kufuata maelekezo haya ili kuhakikisha unaingia kwenye mafunzo bila changamoto yoyote. Tafadhali ratibu safari yako mapema ili kufika kwa wakati!
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako