Tangazo La Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Za Umma 08, 2024 PDF , Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 10 Juni 2023 na 21 Juni 2024 kwamba matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.
Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Hatua za Kuchukua kwa Waombaji Waliofaulu Usaili
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili.
Baada ya siku saba, barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Masharti ya Kuripoti Kituoni
Waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.
Kwa Waombaji Ambao Majina Yao Hayapo Kwenye Orodha
Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili, watambue kuwa hawakufaulu usaili. Hivyo, wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Muhimu
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya kusafiria
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
- Kitambulisho cha Mpiga kura
- Leseni ya Udereva
Tazama Majina Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Za Umma 08, 2024 PDF
Hapa; https://www.ajira.go.tz/baseattachments/placementsattachments/
Kwa ufupi, ni muhimu kufuatilia taratibu hizi ili kuhakikisha kila mmoja anapata taarifa sahihi na kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati.
Soma Zaidi:
Tuachie Maoni Yako