Nafasi Za Kazi Mamlaka Ya Usimamizi Wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) 01-09-2024 Ajira mpya

Tangazo La Nafasi Za Kazi Mamlaka Ya Usimamizi Wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) 01-09-2024 Ajira mpya, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi za kazi mia tatu na hamsini na moja (351) kama ifuatavyo:

1.0 MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA (TAWA)

TAWA ilianzishwa mwaka 2013 kupitia Tangazo la Serikali Na. 124 la tarehe 7 Mei, 2013 ili kuchukua majukumu ya usimamizi wa wanyamapori ambayo awali yalifanywa na Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Ni taasisi inayojitegemea inayohusika na ulinzi, usimamizi na utawala wa rasilimali za wanyamapori nje ya Hifadhi za Taifa na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

1.1 CONSERVATION RANGER III – DEREVA – NAFASI 3

Majukumu:

  • Kuendesha magari ya Mamlaka;
  • Kutunza daftari la safari na kumbukumbu za safari;
  • Kuhakikisha magari yanatembea kwa usalama;
  • Kufanya matengenezo madogo ya magari;
  • Kudumisha usafi wa magari na ratiba ya huduma.

Sifa na Uzoefu:

  • Cheti cha Kidato cha Nne na Leseni ya Udereva Daraja “C au E”.
  • Uhitimu wa Mafunzo ya Msingi ya Udereva kutoka VETA au taasisi inayotambulika.
  • Uzoefu wa kuendesha magari kwa angalau mwaka mmoja bila kusababisha ajali.

Umri:

  • Usiozidi miaka 25.

Malipo:

  • Ngazi ya Mshahara: TAWAS 2.1

1.2 CONSERVATION RANGER III – USIMAMIZI WA WANYAMAPORI – NAFASI 200

Majukumu:

  • Kufanya doria za ulinzi wa wanyamapori;
  • Kukusanya nyara zinazopatikana wakati wa doria;
  • Kurekodi matukio ya ujangili na taarifa za kiikolojia;
  • Kusimamia maeneo ya uhalifu na kukusanya vielelezo na taarifa.

Sifa na Uzoefu:

  • Cheti cha Msingi cha Ufundi katika Usimamizi wa Wanyamapori kutoka chuo kinachotambulika.

Umri:

  • Usiozidi miaka 25.

Malipo:

  • Ngazi ya Mshahara: TAWAS 2.1

1.3 CONSERVATION RANGER III – TEKNISHANI WA WANYAMAPORI – NAFASI 145

Majukumu:

  • Kufanya doria za ulinzi wa wanyamapori;
  • Kukusanya nyara zinazopatikana wakati wa doria;
  • Kurekodi matukio ya ujangili na taarifa za kiikolojia;
  • Kusimamia maeneo ya uhalifu na kukusanya vielelezo na taarifa.

Sifa na Uzoefu:

  • Cheti cha Ufundi katika Usimamizi wa Wanyamapori kutoka chuo kinachotambulika.

Umri:

  • Usiozidi miaka 25.

Malipo:

  • Ngazi ya Mshahara: TAWAS 2.1

1.4 CONSERVATION RANGER II – AFISA MSAIDIZI WA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI – NAFASI 3

Majukumu:

  • Kufanya doria za ulinzi wa wanyamapori;
  • Kukusanya nyara zinazopatikana wakati wa doria;
  • Kurekodi matukio ya ujangili na taarifa za kiikolojia;
  • Kusimamia maeneo ya uhalifu na kukusanya vielelezo na taarifa.

Sifa na Uzoefu:

  • Diploma katika Usimamizi wa Wanyamapori kutoka chuo kinachotambulika.

Umri:

  • Usiozidi miaka 25.

Malipo:

  • Ngazi ya Mshahara: TAWAS 3.1

MASHARTI YA JUMLA:

  1. Waombaji wote wawe raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 25.
  2. Waombaji wawe tayari kuhudhuria na kumaliza mafunzo ya miezi sita ya kijeshi kabla ya kupewa barua ya uteuzi.
  3. Waombaji wawasilishe wasifu wenye taarifa sahihi za mawasiliano.
  4. Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vilivyothibitishwa.
  5. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 13 Septemba, 2024.

Maombi yote yatumwe kupitia tovuti ya ajira: http://portal.ajira.go.tz.