Matokeo ya Mechi ya Taifa stars (Tanzania) vs Guinea Septemba 10, 2024 Live Results, Timu ya Taifa ya Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, itakutana na Guinea katika mchezo muhimu wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 leo, Septemba 10, 2024. Mchezo huu utapigwa saa 1:00 usiku (7:00 PM EAT) katika Uwanja wa Charles Konan Banny, Yamoussoukro, Ivory Coast.
Taifa Stars inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na malengo ya kupata alama tatu muhimu ili kukiuka nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo wa kundi H. Kocha mkuu wa muda, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ameweka wazi kuwa kikosi kimejipanga kuhakikisha kinaondoka na ushindi kwenye mchezo huu wa ugenini.
Takwimu za Mchezo
Hapa kuna muhtasari wa takwimu za mechi zilizopita kati ya Taifa Stars na Guinea:
Tarehe | Michuano | Matokeo |
---|---|---|
27 Januari 2021 | African Nations Championship (CHAN) | Tanzania 2 – 2 Guinea |
2019 | Africa Cup of Nations (AFCON) | Tanzania 0 – 3 Guinea |
2017 | Africa Cup of Nations (AFCON) | Tanzania 0 – 2 Guinea |
Rekodi zinaonyesha kwamba, Guinea imepoteza mechi mbili mfululizo kwa matokeo ya 1-0, kabla ya hapo ilikuwa imeshinda mechi tatu mfululizo. Wakati Stars ikiwa inajiuliza katika lile la ushambuliaji, safu ya ulinzi ya kikosi hicho imeonekana kuwa imara kwa kiasi chake kwani katika mechi hizo 11, imefanikiwa kuondoka na clean sheet sita lakini kwa jumla imeruhusu mabao tisa.
Msimano wa Kundi H
Baada ya mechi za awali, kundi H linaonekana kama ifuatavyo:
Msimamo wa Kundi La Taifa Stars (Tanzania) Kufuzu AFCON 2024/2025
DR Congo inaongoza kundi hili baada ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Guinea. Taifa Stars na Ethiopia wako nafasi ya pili na tatu kila mmoja akiwa na alama moja.
Matokeo Ya Moja Kwa Moja
Unaweza kufuatilia kwenye tovuti ya Hapa LiveScore.
Matarajio ya Mchezo
Katika mchezo wa leo, Taifa Stars inatarajiwa kuingia dimbani kwa mbinu ya kushambulia zaidi, huku ikijua kuwa Guinea itakuwa na njaa ya ushindi. Kocha Morocco amekiri kuwa mchezo utakuwa mgumu lakini wana imani ya kupata matokeo chanya.
Wachezaji wazir Junior, Clement Mzize na Cyprian Kachwele wana jukumu kubwa la kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars katika mchezo huu.
Mchezo huu ni muhimu sana kwa Taifa Stars katika harakati zao za kufuzu AFCON 2025, na mashabiki wanatarajia kuona timu yao ikifanya vizuri. Kwa habari za moja kwa moja kuhusu matokeo ya mchezo huu, unaweza kufuatilia kwenye tovuti ya LiveScore.
Tuachie Maoni Yako