Kozi Za VETA na Gharama zake 2024

Kozi Za VETA na Gharama zake 2024, (Kozi zinazotolewa veta Tanzanaia) Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) nchini Tanzania inatoa kozi fupi mbalimbali zinazolenga kuongeza ujuzi na maarifa ya watanzania.

Kozi hizi zinapatikana katika vyuo mbalimbali vya VETA nchini na zinatoa fursa kwa watu wa rika zote kujifunza stadi mpya ambazo zinaweza kuboresha maisha yao na kusaidia katika kupata ajira.

Aina za Kozi Zitoazo na Gharama Zake

Vyuo vya VETA vinatoa kozi fupi zenye kuanzia wiki mbili hadi miezi sita. Hapa chini ni baadhi ya kozi zinazoonekana kuwa maarufu na zinazotolewa katika vyuo vya VETA pamoja na gharama zake:

Udereva wa Magari ya Abiria (PSV)

    • Muda: Wiki 2
    • Ada: TZS 325,000

Udereva wa Awali (Basic Driving of Motor Vehicle)

    • Muda: Wiki 5
    • Ada: TZS 217,000

Ufundi Bomba (Plumbing and Pipe Fittings)

    • Muda: Miezi 3
    • Ada: TZS 240,000

Ushonaji (Designing Sewing and Cloth Technology)

    • Muda: Miezi 3
    • Ada: TZS 240,000

Umeme wa Majumbani (Electrical Installation)

    • Muda: Miezi 3
    • Ada: TZS 240,000

Matumizi ya Kompyuta (Computer Application)

    • Muda: Miezi 3
    • Ada: TZS 240,000

Soma Zaidi: https://www.veta.go.tz/

Faida za Kozi za VETA Kozi hizi zina faida nyingi kwa washiriki wake:

  • Kuongeza Ujuzi: Washiriki wanapata ujuzi wa vitendo ambao unawawezesha kufanya kazi kwa uhakika na ufanisi.
  • Fursa za Ajira: Kupitia mafunzo haya, washiriki wanapata nafasi nzuri zaidi za ajira kwani wanakuwa na stadi ambazo zinahitajika katika soko la ajira.
  • Kujiendeleza Kitaaluma: Kozi hizi zinatoa msingi mzuri kwa washiriki wanaotaka kujiendeleza zaidi katika taaluma husika.
  • Kupata Cheti: Washiriki wanapata vyeti vinavyotambulika kitaifa ambavyo vinaweza kutumika popote nchini.

Jinsi ya Kujisajili

Ili kujiunga na kozi hizi, washiriki wanatakiwa kulipa gharama ya fomu ya TZS 5,000 kupitia control number ambayo itatolewa na ofisi ya uhasibu ya chuo husika cha VETA. Baada ya hapo, wanaweza kuwasiliana na chuo husika kwa maelezo zaidi na usaidizi wa jinsi ya kujisajili.

Hitimisho

VETA inatoa nafasi nzuri kwa watanzania wote wanaotaka kuongeza ujuzi na maarifa yao kupitia kozi fupi zinazotolewa katika vyuo mbalimbali nchini. Hii ni fursa muhimu kwa wale wanaotaka kuboresha maisha yao na kupata ajira bora. Tunawahimiza watanzania wote kuchangamkia fursa hizi na kujiandikisha kwenye kozi zinazowavutia.

Mawasiliano ya Vyuo vya VETA

Kwa maelezo zaidi na mawasiliano, unaweza kutembelea tovuti ya VETA au kuwasiliana moja kwa moja na vyuo husika kwa namba za simu na barua pepe zilizotolewa kwenye matangazo yao.

Mapendekezo:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.