Form Four Waliochaguliwa Kujiunga Na Vyuo 2024/2025 (Orodha Ya Majina)

Form Four Waliochaguliwa Kujiunga Na Vyuo 2024/2025, Majina ya Waliochaguliwa Mwaka wa masomo wa 2024/2025 umeleta habari njema kwa wanafunzi wa kidato cha nne nchini Tanzania ambao wamechaguliwa kujiunga na vyuo na kidato cha tano. Uteuzi huu unafanywa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na umejumuisha wanafunzi kutoka shule za serikali na zisizo za serikali pamoja na watahiniwa binafsi waliofanya mitihani yao chini ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Takwimu Muhimu

Jumla ya Wanafunzi Waliochaguliwa: 188,787 kati ya 197,426 wahitimu waliofaulu mtihani wa kidato cha nne wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita pamoja na vyuo mbalimbali kwa mwaka 2024.

Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum: Kati ya hao, 812 ni wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Muda wa Kuripoti Shuleni: Wanafunzi wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia tarehe 1 Julai hadi 14 Julai, 2024.

Mchakato wa Uchaguzi

Uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano na vyuo unafanyika baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na NECTA. Wanafunzi waliofaulu mtihani huu wanapewa kipaumbele katika uchaguzi huu. Mchakato huu unazingatia sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 iliyorekebishwa mwaka 2023.

Hatua za Kuangalia Matokeo ya Uchaguzi

Tembelea Tovuti ya TAMISEMI: Unaweza kutembelea TAMISEMI au NECTA ili kuangalia matokeo ya uchaguzi.

Chagua Sehemu ya Uchaguzi wa Kidato cha Tano: Tafuta sehemu inayohusiana na uchaguzi wa kidato cha tano na bofya kiungo husika ili kupata matokeo.

Ingiza Taarifa Zako: Ingiza namba yako ya mtihani au taarifa nyingine zinazohitajika ili kupata matokeo.

Angalia Matokeo: Baada ya kuingiza taarifa, utaweza kuona matokeo yako mtandaoni na shule au chuo ulichopangiwa.

Pakua Maelekezo ya Kujiunga: Ni muhimu kupakua na kusoma maelekezo ya kujiunga na shule au chuo ulichopangiwa.

Mikoa na Shule Zilizochaguliwa

Mkoa Mkoa Mkoa
Arusha Dar es Salaam Dodoma
Geita Iringa Kagera
Katavi Kigoma Kilimanjaro
Lindi Manyara Mara
Mbeya Morogoro Mtwara
Mwanza Njombe Pwani
Rukwa Ruvuma Shinyanga
Simiyu Singida Songwe
Tabora Tanga
Kwa maelezo zaidi kuhusu majina ya waliochaguliwa na vyuo vya umma na serikali, unaweza kutembelea tovuti za TAMISEMINACTVET.
Mapendekezo: