Jinsi ya Ku- confirm Mwajiri ajira Portal (Kada ya Elimu N.K), Ajira Ualimu utumishi Angalieni status zenu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwajulisha wale wote walioomba kazi ya kufundisha katika Mikoa tofauti tofauti kuwa, imetoa siku tatu kuanzia terehe 14 mpaka16 Septemba, 2024 kwa ajili ya kuhuisha (update) taarifa zao za Mkoa ulioomba kufanya kazi katika mfumo wa Ajira Portal endapo unasomeka tofauti na Mkoa ambao ungependa kufanya kazi.
Aidha, Hakikisha Mkoa unaosomeka katika eneo la Mwajiri “Employer” ndilo ulilo omba kama ni tofauti unapaswa kubadilisha kwenye mfumo kwani sehemu hii ndio itakayopelekea kupangiwa kituo cha Usaili wa Mahojiano na hatimaye kupangiwa kituo cha kazi.
Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni sikivu, imesikia maombi yenu hivyo, imetoa siku tatu tu kwa ajili ya kuhuisha taarifa zenu. Changamoto hii imejitokeza wakati wa kutuma maombi ya kazi ambapo waombaji wengi walijaziwa taarifa zao na ndugu, jamaa na hata wahudumu wa ‘stationaries’ na hamkupata nafasi ya kuhakiki kilichojazwa kama ni sahihi.
Kutokana na changamoto hiyo, ofisi inawasisitiza watafuta fursa za ajira kuwa makini wakati wote wa ujazaji wa taarifa katika mfumo wa Ajira Portal na kuhakiki taarifa zao ili kuepuka usumbufu.
Ili kuweza kufanikisha kuhuisha taarifa zako katika mfumo wa Ajira Portal fuata maelekezo yafuatayo;
- Ingia katika akaunti yako ya Ajira Portal;
- Nenda Sehemu iliyoandikwa “My APPLICATIONS” kwenye Akaunti yako ya Ajira Portal kisha bonyeza sehemu hiyo;
- Chagua Sehemu iliyoandikwa “SELECT EMPLOYER” kisha bonyeza hapo na kuchagua mkoa ambao ungependa kufanya kazi;
- Kisha ujumbe utakuja “CONFIRM EMPLOYER” wa kukutaka Uthibitishe Mwajiri “Employer” kwa Maana ya mkoa uliochagua kuwa ni sahihi na itakulazimu ubonyeze sehemu iliyoandikwa SUBMIT kwa ajili ya kuwasilisha;
- Kisha utaona ujumbe umeandikwa “EMPLOYER CONFIRMED SUCCESSFULLY”. Hii itamaanisha kuwa umefanikiwa kubadilisha/kuhuisha na kuchagua mkoa ambao ungependa kufanya
Ukimaliza ukienda katika Akaunti yako utaweza kuona mkoa ulio chagua na mkoa huo ndio utapelekea kupangiwa kituo cha kazi baada ya kufaulu usaili wa mahojiano.
Vile vile waomba kazi wanatakiwa kuhuisha taarifa zao katika sehemu ya “Current address” sehemu iliyoandikwa “current resident region” na “current resident district” taarifa zinazo onekana sehemu hii ndizo zitakazo tumika kupanga sehemu ya kufanyia usaili wa Kuandika/Mchujo (Aptitude Test)
Mapendekezo:
Nini Kipya Huku ajira portal (walimu)
Ajira Portal Login (Mfumo wa Maombi ya ajira)
Walioitwa kwenye interview Utumishi 2024 (Usaili) Ajira Portal
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa umma itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na vilevile kusikiliza na kuyafanyia kazi maoni mbalimbali yanayotolewa na wadau kwa lengo la kuboresha zaidi mchakato wa ajira.
Lynn Chawala
My application
Good
Ajira Portal News Habari Mpya na Miongozo
Nachokijua Kuhusu Ajira Portal
Ajira Portal News Habari Mpya na Miongozo (Ajira Portal Login) and Updates Ajira Portal ni mfumo maalumu ulioundwa na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa ajili ya kusimamia mchakato wa ajira serikalini. Mfumo huu umeundwa ili kurahisisha utoaji wa ajira kwa uwazi, ufanisi na kwa kuzingatia weledi.
Kuna News Gani Ajira Portal?
Kupitia Ajira Portal, waombaji wa nafasi za ajira wanaweza kuwasilisha maombi yao, kuhuisha taarifa zao, na kufuatilia hatua mbalimbali za mchakato wa maombi yao.
Jinsi ya Kuingia na Kuhuisha Taarifa (Ajira Portal Login)
Unapotumia Ajira Portal, hatua ya kwanza ni kuhakikisha kuwa umehuisha taarifa zako binafsi kwa usahihi. Hii ni muhimu kwa sababu taarifa hizi ndizo zitakazotumika katika mchakato mzima wa maombi yako ya ajira Kupitia https://portal.ajira.go.tz/.
Hatua za kufuata:
Ingiza namba yako ya utambulisho wa Taifa (NIN) kutoka NIDA.
Mfumo utakuthibitisha kupitia maswali machache ili kuendana na rekodi za NIDA.
Baada ya kuthibitishwa, taarifa zako kutoka NIDA zitaingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa Ajira Portal.
Hakikisha umejaza taarifa zote muhimu kama jina kamili, tarehe ya kuzaliwa, na jinsia, kisha bofya sehemu ya Hifadhi (Save).
Anwani na Mawasiliano (Contact Details) Ajira Portal
Waombaji wa ajira wanashauriwa kuingiza anwani zao kwa usahihi ili waweze kufikiwa kwa urahisi endapo wataitwa kwenye hatua ya usaili au kupewa taarifa zingine muhimu.
Mambo ya kuzingatia:
Ingiza anuani kamili ya makazi, namba ya simu, na barua pepe inayotumika.
Unapotumia namba ya simu, hakikisha ni ile inayopatikana wakati wote kwani taarifa za usaili zinaweza kutumwa kupitia njia hii.
Kuhusu Kuelewa ‘STATUS’ ya Maombi Yako ya Kazi
Waombaji wanaweza kuona maendeleo ya maombi yao kwa kuingia kwenye sehemu ya My Application baada ya ku-login kwenye akaunti zao. Katika eneo hili, unaweza kufuatilia kama maombi yako yamepokelewa, umekubaliwa au umekataliwa kwa usaili, na sababu za kutokuitwa endapo hukuchaguliwa. Mfumo huu ni rahisi na unakupa mrejesho wa haraka kuhusu hatua ya maombi yako.
Mawasiliano ya ajira portal ni yapi?
Contacts: President’s Office,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. BOX 2320,
Dodoma.
katibu@ajira.go.tz
+255 (26) 2963652