Wanasayansi 10 bora Duniani (Watu wenye iq kubwa duniani), Watu wenye akili nyingi na mchango mkubwa katika sayansi ni muhimu katika maendeleo ya jamii. Hapa kuna orodha ya wanasayansi kumi bora duniani, wakitambulika kwa uwezo wao wa kiakili na uvumbuzi wao.
1. Terence Tao
- IQ: 230
- Maelezo: Mwanahisabati kutoka Marekani, Terence aliweza kufanya hisabati akiwa na miaka 2 na alipata PhD akiwa na miaka 20. Amepata tuzo nyingi, ikiwemo Medali ya Fields mwaka 2006.
2. Christopher Hirata
- IQ: 225
- Maelezo: Mnajimu anayefanya kazi na NASA, alishinda tuzo ya Mwanahisabati Bora wa Dunia akiwa na miaka 13 na alipata PhD akiwa na miaka 22.
3. Kim Ung-Yong
- IQ: 210
- Maelezo: Alijulikana kwa uwezo wake wa kujifunza lugha mbalimbali akiwa mtoto mdogo, akijua Kijapani, Kikorea, Kiingereza, na Kijerumani kabla ya umri wa miaka mitatu.
4. Rick Rosner
- IQ: 192
- Maelezo: Mwandishi wa kipindi cha Jimmy Kimmel ambaye awali alikuwa dansa wa club za usiku. IQ yake ilishangaza wengi kutokana na kazi alizofanya.
5. Garry Kasparov
- IQ: 192
- Maelezo: Mchezaji maarufu wa chess ambaye pia anajihusisha na siasa. Alitaka kugombea urais wa Urusi.
6. Galileo Galilei
- IQ: 185
- Maelezo: Mwanasayansi maarufu kwa ugunduzi wake katika anga, hisabati, na fizikia. Alijulikana sana kwa kubaini umbo la dunia.
7. James Woods
- IQ: 180
- Maelezo: Mchezaji filamu ambaye ameshinda tuzo nyingi za Academy. Alionyesha uwezo mkubwa wa hisabati akiwa mdogo.
8. Judit Polgar
- IQ: 170
- Maelezo: Mwanamke pekee kwenye orodha hii, alishinda mechi dhidi ya mshindi wa dunia wa chess akiwa na miaka 15.
9. Andrew Wiles
- IQ: 170
- Maelezo: Mwanahisabati kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, alijulikana kwa kutatua “Fermat’s Last Theorem” na kushinda tuzo ya Abel Prize mwaka 2016.
10. Albert Einstein
- IQ: 160
- Maelezo: Mwanafizikia maarufu anayejulikana kwa mchango wake mkubwa katika sayansi na nadharia za uhusiano, jina lake limekuwa alama ya ujuzi mkubwa wa akili.
Orodha hii inaonyesha wanasayansi ambao wamechangia pakubwa katika maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani, huku wakionyesha uwezo wao wa kiakili unaovuka mipaka ya kawaida.
Tuachie Maoni Yako