Vigezo Vya Kupata Mkopo Ngazi Ya Diploma 2024/2025 HESLB, Vigezo vya kupata mkopo ngazi ya diploma 2024 2025 pdf. Wanafunzi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu kwa ngazi ya stashahada, habari njema ni kuwa dirisha la maombi ya mkopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025 litafunguliwa.
Wanafunzi wanapaswa kuzingatia udahili wa muhula wa MACHI NA OKTOBA. Kwa muhula wa Oktoba, dirisha litafunguliwa kuanzia tarehe 1 Juni, 2024 hadi tarehe 31 Agosti, 2024.
Sifa za Kuomba Mikopo
Ili kuweza kuomba mkopo, mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
Vigezo vya Msingi
- Awe Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 35 wakati wa kuomba mkopo.
- Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu inayotoa elimu ya ngazi ya kati nchini.
- Awe amekamilisha na kuwasilisha maombi ya mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS).
- Asiwe na ajira au mkataba wa kazi serikalini au sekta binafsi.
- Awe amehitimu elimu ya Kidato cha Nne (CSEE), Cheti (astashahada), au Kidato cha Sita (ACSEE) ndani ya miaka mitano, yaani kati ya mwaka 2020 hadi 2024.
- Kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo, matokeo yao yanayomwezesha kuendelea na masomo yanapaswa kuwasilishwa Bodi ya Mikopo kupitia Afisa Mikopo au uongozi wa Chuo.
Hali ya Kijamii na Kiuchumi
- Uyatima; aliyefiwa na mzazi au wazazi.
- Familia au kaya ya kipato duni inayofadhiliwa na Mifuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) au taasisi nyingine za kitaifa zinazotoa ufadhili kwa kaya zenye vipato duni.
- Ulemavu wa mwombaji au wazazi wake.
Upangaji wa Mikopo
Upangaji wa mikopo utafuata vipaumbele vifuatavyo:
- Mwanafunzi mwenye udahili kwenye programu zilizoainishwa katika Mwongozo.
- Hali ya kijamii kama ilivyoelezwa.
Nyaraka za Kuambatisha
Wakati wa maombi ya mkopo, ni muhimu kuambatisha nyaraka zifuatazo:
- Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika.
- Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima.
- Barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kuzaliwa kwa waombaji waliozaliwa nje ya nchi.
- Fomu ya Kuthibitisha Ulemavu iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya au Mkoa.
- Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Wanafunzi wanashauriwa kufuata mchakato huu kwa umakini ili waweze kufanikiwa katika maombi yao ya mikopo. Kumbuka, elimu ni msingi wa maendeleo, na uwekezaji katika elimu yako ni uwekezaji katika siku zijazo.
Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Soma Zaidi:
Tuachie Maoni Yako