Tuzo za TMA 2024 Tanzania Music Award (TMA)

Tuzo za TMA 2024, Kamati ya Tanzania Music Award (TMA) leo August 29,2024 imeanza kutangaza Nominees wanaowania tuzo za muziki Nchini kwa kuanza na category tatu ambazo ni Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, wimbo bora wa taarabu wa mwaka na wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi.

Wimbo bora wa taarabu wa mwaka kuna Watu na Viatu ya Malkia Layla Rashid, Hatuachani ya Amina Kidevu, Bila Yeye Sijiwezi ya Mwinyi Mkuu, Sina Wema ya Mwasiti Mbwana na DSM Sweetheart ya Salha.

Wimbo bora Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi kuna People ya Libianca, American Love ya Qing Madi, Lonely at the Top ya Asake, Unavailable ya Davido ft Musa Keys na Mnike ya Tyler ICU.

Kwa upande wa Mwanamuziki bora wa mwaka wa kiume kuna Marioo kupitia wimbo wa Shisha , Diamond Platnumz kupitia Shuu, Harmonize kupitia Single Again , Alikiba kupitia Sumu na Jay Melody kupitia wimbo wa Nitasema

Kamati ya Tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema category nyingine zitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifumgulowa rasmi September 3.

Kamati ya TMA imeendelea kutaja Wasanii wanaowania vipengele tofautitofauti na leo August 30,2024 vimetajwa vipengele vingine ikiwemo kipengele cha Tanzania Global Icons Award (Mtanzania anayeipeperusha vema bendera ya Tanzania Kimataifa) ambapo wanaowania ni Mchezaji Mbwana Samatta, Mwanamitindo Flaviana Matata , Wanasarakasi Ramadhan Brothers, pamoja na Anisa Mpungwe na Clara Luvanga.

Kipengele kingine ni Best Dance Music Song of The Year ambacho kina Diamond ft Koffie Olomide kupitia wimbo wa Achii, pia kuna Malaika Band wimbo wa Kanivuruga, Melody Mbassa wimbo wa Nyoka na Twanga Pepeta kupitia wimbo wa Mmbea.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by millardayo (@millardayo)


Kipengele kingine ni Best Traditional Musician of The year (Mwanamuziki Bora wa Nyimbo za Asili) ambapo yupo Erica Lulakwa, Elizabeth Maliganya, Sinaubi Zawose, Ngapi Group na Wamwiduka Band.

Kamati ya tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha imesema category nyingine zitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifunguliwa rasmi September 3,2024.

Kamati ya TMA imeendelea kutaja Wasanii wanaowania vipengele tofautitofauti ikiwemo kipengele cha Msanii Bora wa HipHop ambapo majina yanayowania tuzo ni Joh Makini, Stamina, Young Lunya, Kontawa na Rosa Ree.

Kipengele kingine ni cha wimbo bora wa HipHop ambapo zimeingia ngoma za Bobea ya Joh Makini , Machozi ya Stamina, Stupid ya Lunya, Current Situation ya Country Wizzy na Uongo ya Rapcha.

Kamati hiyo ya TMA inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha wamesema category nyingine zitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifumguliwa rasmi September 03,2024

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.