Tangazo la kuripoti shule ya Polisi Moshi 2024

Tangazo la kuripoti shule ya Polisi Moshi 2024, Tangazo La Kuripoti Shule Ya Polisi Moshi Kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania – Septemba 23, 2024. Katika maandalizi ya kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania, vijana waliochaguliwa wanatakiwa kufuata taratibu maalum za kuripoti ili kushiriki mafunzo ya Shule ya Polisi Moshi. Taarifa hii ni muhimu kwa kila kijana aliyechaguliwa kuhakikisha anatimiza wajibu wake kama inavyotakiwa.

Ratiba na Maelekezo ya Kuripoti

Mkuu wa Jeshi la Polisi anatoa maelezo yafuatayo:

1. Tarehe ya Kuripoti

Vijana wote wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kati ya tarehe 30 Septemba 2024 hadi 02 Oktoba 2024. Ukichelewa kuripoti baada ya tarehe 02 Oktoba, utachukuliwa kuwa umejiondoa kwenye mafunzo.

2. Vijana Waliofanyiwa Usaili Dar es Salaam

Wale waliochaguliwa kupitia Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) Dar es Salaam wanatakiwa kuripoti tarehe 30 Septemba 2024 saa 12:00 asubuhi, eneo la Polisi Barracks Barabara ya Kilwa, karibu na Hospitali Kuu ya Polisi. Safari ya kuelekea Shule ya Polisi Moshi itaanza hapo.

3. Vijana Waliofanyiwa Usaili Mikoani

Waliopitia usaili katika mikoa ya Tanzania Bara wanapaswa kuripoti tarehe 29 Septemba 2024 saa 2:00 asubuhi kwa Makamanda wa Polisi wa mikoa husika kwa maelekezo zaidi juu ya safari ya kuelekea Moshi.

4. Vijana Kutoka Zanzibar

Kwa vijana waliofanyiwa usaili Zanzibar (Unguja na Pemba), wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 29 Septemba 2024 kwa ajili ya kupata utaratibu wa safari.

5. Vifaa Muhimu vya Kuleta

Vijana wote waliochaguliwa wanapaswa kuwa na vifaa vifuatavyo wanaporipoti:

Kifaa Maelezo
Track suit Rangi ya bluu yenye ufito mweupe. Fulana nyeupe isiyo na maandishi, raba, soksi nyeusi, na bukta mbili za bluu kwa ajili ya mazoezi.
Sanduku la chuma Rangi ya bluu (tranka).
Chandarua na Shuka Chandarua cheupe cha duara, shuka mbili za rangi ya light blue, na blanket moja la kijivu (sio duveti).
Vifaa vya Usafi Jembe lenye mpini, reki, panga, fagio la chelewa, ndoo mbili ndogo.
Bima ya Afya au Tsh. 50,400 Kadi ya bima ya afya (NHIF) au fedha taslimu kwa ajili ya bima ya afya kwa wasio na kadi.
Vyeti Halisi Vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa Taifa, nakala za vyeti, na picha za passport size 6.
Fedha ya kujikimu Fedha ya matumizi binafsi wakati wa mafunzo.

6. Marufuku ya Simu za Mkononi

Ni marufuku kuripoti na simu ya mkononi. Yeyote atakayepatikana na simu atachukuliwa kuwa ametenda utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja.

7. Baada ya Tarehe 02 Oktoba

Kwa vijana watakaochelewa kuripoti baada ya tarehe 02 Oktoba, hawatapokelewa na watahesabika wamejiondoa kwenye mafunzo ya Polisi.

8. Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa

Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Polisi imeambatanishwa kwenye tangazo hili. Unaweza kupakua orodha ya majina hapa.


Imetolewa na: Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.
23 Septemba 2024.

Tafadhali hakikisha unafuata maelekezo yote kwa usahihi ili kuepuka changamoto zozote!

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.