Tangazo La Kuitwa Kazini Taasisi Mbalimbali Za Umma 18-08-2024 Majina, Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 10-06-2023 na tarehe 21-06-2024 kuwa matokeo ya usaili huo yamekamilika.
Waombaji waliofaulu usaili wameteuliwa kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi kwenye taasisi mbalimbali za umma. Orodha ya majina yao imeorodheshwa katika tangazo hili, ikijumuisha pia baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
- Tarehe: 18-08-2024
- Kumb. Na.: JA.9/18/01/26
- Mtoa Taarifa: Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Jinsi ya Kupata Barua za Kupangiwa Kituo cha Kazi:
Waombaji waliofaulu wanatakiwa kufika katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, ili kuchukua barua zao ndani ya siku saba (7) kutoka tarehe ya tangazo hili. Baada ya siku saba, barua ambazo hazitachukuliwa zitatumwa kwa wahusika kupitia anuani zao za Posta.
Maagizo ya Kuripoti Kituo cha Kazi:
Waombaji waliofaulu na kupangiwa vituo vya kazi wanapaswa kuripoti kwa mwajiri ndani ya muda ulioainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi.
Wakiwa wanaripoti, wanapaswa kubeba vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira rasmi. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika orodha hii, wasisite kuomba nafasi nyingine zitakapotangazwa.
Wakati wa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi, waombaji wanapaswa kuwasilisha kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:
- Kitambulisho cha Uraia
- Hati ya Kusafiria
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
- Kitambulisho cha Mpiga Kura
- Leseni ya Udereva
Kwa maelezo zaidi kuhusu mchakato huu, unaweza kutembelea tovuti rasmi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma au kufika moja kwa moja katika ofisi zao.
PDF Ya Majina Hapo Chini:
TANGAZO LA KUITWA KAZINI TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA 18-08-2024
Tuachie Maoni Yako