Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema imepokea maombi ya leseni chini ya mfumo wa leseni kutaniko kutoka kwa Waombaji watatu wakiwemo Starlink Satellite Tanzania Limited kampuni inayomilikiwa na Tajiri namba moja Duniani ambaye ni Boss wa Makampuni ya SpaceX, Tesla na X (zamani Twitter), Elon Musk, ambaye ameomba leseni ya kitaifa ya miundombinu na leseni ya kitaifa ya huduma ya mifumo tumizi na kwenye taarifa hiyo Wanahisa wa kampuni hiyo wanatajwa kuwa ni Starlink Holdings Netherlands B.V na SpaceX Netherlands B.V.
Taarifa iliyotolewa leo November 15,2024 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabir Bakari, imesema “Kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta, Sura 306 ya sheria za Tanzania, maoni ya kimaandishi yanakaribishwa kutoka kwa yeyote kuhusiana na utoaji wa leseni kwa waombaji yafike TCRA ndani ya siku 14 tangu siku ya kutoka tangazo hili, maoni yatakayopokelewa yatazingatiwa na TCRA itakapokuwa inayafanyia kazi ombi hili”
Itakumbukwa February 24,2024 aliyekuwa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye alisema Serikali ya Tanzania imeshatoa majibu kwa kampuni ya Starlink na vikao vinaendelea ili wakamilishe documents na waruhusiwe kuanza huduma zao Tanzania na kusema hakuna ukweli kwamba Starlink wanahujumiwa.
Waziri Nape alitoa kauli hiyo baada ya Elon Musk kusema kilichobaki kwenye mpango wake wa kuuleta mradi wa Starlink Tanzania ni kibali tu kutoka kwenye Serikali ya Tanzania ambapo Nape alinukuliwa akisema “Nchi ina sheria katika kusajili Watoa huduma za mawasiliano, Starlink walijaza maombi yao November mwaka jana na kuna vikao vilfanyika, ndio maana Elon alipotweet nikasema nadhani unakumbuka Mamlaka za Tanzania zilikutaka tume document na vikao vinaendelea, sisi kama Wasimamizi wa Sekta wakikamilisha document zao wanapewa tu kibali”
“Nashangaa Watanzania wanakuja juu ‘unajua huyu kapewa
hela, huyu kafanya hivi, wanataka kumuhujumu (Elon), huyu kafanya vile’, Mimi nadhani sio sawa, kasema hadharani sisi tumesema hadharani, na kuna vikao vinaendelea, wakikamilisha wataruhusiwa hatuna sababu ya kuwazuia”
Tuachie Maoni Yako