Sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu 2024/2025

Sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu 2024/2025, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza nafasi za mafunzo ya ualimu katika ngazi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Waombaji wanastahili kuwa na sifa zifuatazo:

Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 02)

  • Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali.
  • Walimu waliohitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi au Elimu Maalumu. Waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa kwa sifa hii watapangwa kwenye michepuo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada.

Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA

  • Wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni: Basic Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science.

Vyeti vya Ualimu katika Elimu ya Msingi na Msingi

  • Wahitimu wa kidato cha nne wenye matokeo ya Daraja la I-III.

Stashahada ya Ualimu katika Elimu ya Sekondari Stashahada ya Sayansi, Biashara na Hisabati (miaka 03)

  • Wahitimu wa kidato cha nne wenye daraja la I-III kwa ngazi ya daraja la “C” katika masomo matatu kati ya hayo, mawili ambayo ni mahususi kwa masomo ambayo mwombaji anaomba kusoma.

Waombaji wa mafunzo ya ualimu katika Vyuo vya Serikali wametakiwa kujisajili na kutuma maombi kwa njia ya kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (tcm.moe.go.tz).

Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja kwenye vyuo wanavyovipenda na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji kwenye Baraza la Mitihani la Tanzania kwa uhakiki.

Majibu kwa waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia “akaunti” itakayotumiwa na mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia tarehe 25/08/2024) na katika Vyuo vya Ualimu walichaguliwa.

Soma Zaidi:

Nimebobea kwenye uandaaji wa makala za mtandaoni, Makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.