Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Biashara CBE

Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Biashara CBE, Hapa ni sifa muhimu za kujiunga na Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa mwaka:

Astashahada (Certificate Programmes) NTA Level 4 (Mwaka 1)

  • Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (IV) na kupata ufaulu wa angalau masomo 4 kwa kiwango cha kuanzia D (4D’s).
  • Muombaji wa kozi ya Uhasibu anapaswa awe amefaulu Hesabu kidato cha nne kuanzia kiwango cha D.
  • Muombaji wa kozi ya Mizani na Vipimo anapaswa awe amefaulu Hesabu au Fizikia kidato cha nne kuanzia kiwango cha D.
  • Au awe amesoma na kuhitimu NABE II kwa ufaulu wa angalau alama 4.

Stashahada (Diploma Programmes) NTA Level 5-6 (Miaka 2)

  • Mwombaji awe amemaliza kidato cha sita (VI) na kupata ufaulu wa angalau masomo 6 kwa kiwango cha kuanzia C (6C’s) katika somo la Hesabu au Fizikia.
  • Au awe amesoma na kuhitimu Astashahada (Certificate) ya CBE au taasisi nyingine inayotambuliwa.

Shahada (Bachelor Degrees) NTA Level 7-8 (Miaka 4)

  • Mwombaji awe amemaliza kidato cha sita (VI) na kupata ufaulu wa angalau masomo 6 kwa kiwango cha kuanzia C (6C’s) katika somo la Hesabu au Fizikia.
  • Au awe amesoma na kuhitimu Stashahada (Diploma) ya CBE au taasisi nyingine inayotambuliwa.

Maombi yote ya kujiunga na chuo yanafanyika chuoni au kwa njia ya mtandao (Online Application) kupitia tovuti ya chuo http://www.cbe.ac.tz. Dirisha la maombi la muhula wa Septemba limefunguliwa.

Soma Sifa Zaidi:
Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.