Ratiba ya SGR Kutoka Dar es Salaam Kwenda Dodoma 2024

Ratiba ya SGR Dar es Salaam to Dodoma, Ratiba ya Treni ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Safari ya treni ya SGR (Standard Gauge Railway) kati ya Dar es Salaam na Dodoma ni njia bora kwa wale wanaotaka kusafiri haraka na kwa urahisi. Katika blogu hii, tutakupa ratiba kamili ya treni, ili uweze kupanga safari yako vizuri.

Ratiba ya Treni za Haraka (Express)

Dar es Salaam hadi Dodoma:

  • DSM: Kuondoka saa 12:00 asubuhi
  • Morogoro (MOR): Kuwasili saa 1:37 asubuhi, kuondoka saa 1:42 asubuhi
  • Dodoma (DOM): Kuwasili saa 3:25 asubuhi

Dodoma hadi Dar es Salaam:

  • DOM: Kuondoka saa 11:30 asubuhi
  • Morogoro (MOR): Kuwasili saa 1:10 asubuhi, kuondoka saa 1:15 asubuhi
  • DSM: Kuwasili saa 2:45 asubuhi

Ratiba ya Treni za Kawaida (Ordinary)

Dar es Salaam hadi Dodoma:

  • DSM: Kuondoka saa 12:55 jioni
  • Morogoro (MOR): Kuwasili saa 2:40 usiku, kuondoka saa 2:45 usiku
  • Dodoma (DOM): Kuwasili saa 4:35 usiku

Dodoma hadi Dar es Salaam:

  • DOM: Kuondoka saa 11:30 jioni
  • Morogoro (MOR): Kuwasili saa 1:18 usiku, kuondoka saa 1:25 usiku
  • DSM: Kuwasili saa 3:05 usiku

Ratiba ya Treni ya Kawaida Dar es Salaam – Morogoro

Dar es Salaam hadi Morogoro:

  • DSM: Kuondoka saa 3:30 asubuhi, kuwasili saa 5:10 asubuhi
  • DSM: Kuondoka saa 10:00 jioni, kuwasili saa 11:40 jioni
KITUO KUONDOKA KITUO KUWASILI
DSM 3:30 Asbh MOR 5:10 Asbh
MOR 3:50 Asbh DSM 5:40 Asbh
DSM 10:00 Jioni MOR 11:40 Jioni
MOR 10:20 Jioni DSM 12:10 Jioni

Faida za SRG kwa Uchumi wa Tanzania

Ujenzi wa SGR unatarajiwa kuleta manufaa mbalimbali, ikiwemo:

  1. Ongezeko la Usafirishaji wa Mizigo: Reli hii itabeba mzigo wa hadi tani 10,000 kwa mkupuo, sawa na uwezo wa maroli 500. Hii itarahisisha usafirishaji wa bidhaa.
  2. Uokoaji wa Muda: Itasaidia kupunguza muda wa usafiri kwa abiria na mizigo, hivyo kukuza uchumi wa watu binafsi na taifa kwa ujumla.
  3. Ongezeko la Ajira: Mradi huu utaongeza nafasi za ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.
  4. Oboreshaji wa Huduma za Kijamii: Ujenzi wa shule, vituo vya afya, na barabara katika maeneo yanayopitiwa na mradi utasaidia kuboresha huduma za jamii.
  5. Kuchochea Maendeleo: Reli hii itachochea maendeleo katika sekta za kilimo, biashara, madini, na viwanda katika maeneo inayopita, pamoja na nchi jirani kama Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, na DRC.
  6. Kupunguza Gharama za Usafirishaji: SRG itasaidia kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.

Mpangilio wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa

Ujenzi wa reli hii unafanywa kwa awamu tano:

  • Awamu ya 1: Dar es Salaam – Morogoro (Km 300)
  • Awamu ya 2: Morogoro – Makutupora (Km 442)
  • Awamu ya 3: Makutupora – Tabora (Km 294)
  • Awamu ya 4: Tabora – Isaka (Km 130)
  • Awamu ya 5: Isaka – Mwanza (Km 249)

Awamu ya kwanza ilizinduliwa na Rais wa awamu ya tano, Dr. John Pombe Magufuli, tarehe 12 Aprili 2017, na ujenzi unaendelea chini ya mkandarasi YAPI MERKEZI kutoka Uturuki.

Usalama na Uhifadhi wa Mazingira

Ujenzi wa SRG unazingatia usalama wa watu na mali zao. Sehemu za mwingiliano wa magari na reli zitakuwa na kivuko cha juu au chini, na uzio utajengwa ili kulinda watu na wanyama. Pia, elimu kuhusu usalama itatolewa mara kwa mara kwa umma.

Utwaaji wa Ardhi na Malipo kwa Waathirika

Kulingana na sheria ya ardhi ya mwaka 1999 na sheria ya tathmini ya mwaka 2016, maeneo yote yanayopitiwa na mradi ambayo hayamilikiwi na TRC yatafanyiwa tathmini, kutwaliwa, na wamiliki wa maeneo hayo watalipwa fidia.

Soma Zaidi:

Mradi wa SGR ni hatua muhimu katika kuboresha sekta ya usafirishaji nchini Tanzania. Ujenzi wa reli hii ya kisasa utachangia katika ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira, na kuboresha maisha ya wananchi. Kwa hivyo, ni muhimu kuunga mkono jitihada hizi za maendeleo ili kufikia malengo ya nchi.

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.