Namba ya NIDA Online (Mfumo wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa), Jinsi Ya Kuomba Kitambulisho cha Taifa Mtandaoni (NIDA) Katika makala hii, tutazungumzia jinsi ya kuomba Kitambulisho cha Taifa (NIDA) mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya NIDA https://eonline.nida.go.tz. Mfumo huu unawaruhusu waombaji wa vitambulisho vya kitaifa kujaza fomu za maombi kwa njia ya elektroniki kutoka mahali popote.
Hatua za Kuomba Kitambulisho cha Taifa Mtandaoni
- Tembelea Tovuti ya NIDA Fungua kivinjari chako na nenda kwenye tovuti ya NIDA: eonline.nida.go.tz.
- Jaza Fomu ya Maombi
- Fuata maagizo kwenye tovuti ili kujaza fomu ya maombi.
- Hakikisha una barua pepe ambayo utatumia kujiandikisha na kupokea kiungo cha kukamilisha usajili wako.
- Taarifa Zinazohitajika Unahitaji kuwa na hati mbili zinazothibitisha utambulisho wako, kama cheti cha kuzaliwa. Hati hizi zinapaswa kuwa katika format ya PDF (siyo zaidi ya ukurasa mmoja kwa kila kiambatisho) au picha za JPG au PNG.
- Weka Taarifa Sahihi
- Jaza nambari yako ya simu ili waweze kuwasiliana nawe.
- Ikiwa ulizaliwa mwaka 1980 na kuendelea, lazima uambatishe cheti cha kuzaliwa.
- Kwa waliozaliwa kabla ya 1980, ni lazima uambatishe cheti cha kuzaliwa au “Affidavit”.
- Jaza Taarifa za Wazazi
- Ni muhimu kujua majina ya baba na mama yako.
- Ikiwa wazazi wako wana Namba za Kitambulisho cha Taifa (NIN), fanya nakala za hati hizo.
- Jaza Taarifa za Makazi
- Jaza nambari ya nyumba, mtaa na kata unayoishi.
- Kwa Watanzania walioko nje ya nchi, ni lazima kupata uthibitisho wa makazi kutoka ofisi ya ubalozi ya Tanzania.
- Tuma Maombi Yako
- Baada ya kujaza fomu, print fomu hiyo na upeleke ofisi ya NIDA ya karibu (katika wilaya yako) ili kukamilisha mchakato wa usajili wa alama za kibaiometric.
- Pata Stika na Saini
- Hakikisha fomu yako imewekwa stika na saini na mwenyekiti wa serikali ya mitaa unayoishi.
- Tembelea Ofisi ya NIDA
- Tembelea ofisi ya NIDA iliyoko katika wilaya yako na upeleke fomu iliyokamilika pamoja na nakala za hati ulizopakia wakati wa usajili.
Nyaraka Zinazohitajika kwa Waombaji wa Kitambulisho cha Taifa
- Kwa Raia:
- Cheti cha kuzaliwa.
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kiapo cha mzazi mmoja.
- Nakala ya kitambulisho cha taifa cha mzazi kama raia wa kurithi.
- Kwa Wakaazi wa Kisheria:
- Nambari ya pasipoti.
- Leseni ya kuishi au leseni ya kazi.
Mawasiliano ya NIDA
Ikiwa unahitaji maelezo zaidi, usisite kuwasiliana na NIDA kupitia:
Simu: 0689088888, 0687088888, 0777740008, 0777740006, 0735201020, 0736201020, 0743000058, 0752000058, 0677146667, 0677146666
Barua pepe: info@nida.go.tz
Kuomba Kitambulisho cha Taifa kupitia mtandao ni mchakato rahisi na wa haraka. Hakikisha unafuata hatua zote kwa makini ili uweze kupata kitambulisho chako bila shida. Tembelea tovuti rasmi ya NIDA kwa maelezo zaidi na hatua za usajili.
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako