Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chamwino 25-08-2024

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chamwino 25-08-2024, Kufuatia idhini ya utekelezaji wa ajira mpya kwa mwaka wa fedha 2023/2024, kwa kibali chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25-06-2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kujaza nafasi za kazi tajwa hapa chini kwa njia ya mfumo wa Ajira Portal. Nafasi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:

1.0 Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja II – Nafasi 6

1.1 Kazi na Majukumu:

  1. Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista.
  2. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi.
  3. Kusambaza majalada kwa Watendaji.
  4. Kupokea majalada kwa Watendaji.
  5. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
  6. Kurudisha majalada kwenye shabaka au kabati la majalada.
  7. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi.

1.1.1 Sifa za Mwombaji:

  • Kuajiriwa mhitimu wa Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI).
  • Stashahada (NTA level 6) katika fani ya utunzaji kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
  • Ujuzi wa Kompyuta.

1.1.2 Ngazi ya Mshahara:

  • Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C.

1.2 Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 1

1.2.1 Kazi na Majukumu:

  1. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.
  2. Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa.
  3. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake, na ratiba za kazi zingine.
  4. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
  5. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa waliokatika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
  6. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
  7. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
  8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
  9. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

1.2.2 Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha IV au VI.
  • Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
  • Ujuzi wa Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (maneno 100 kwa dakika).
  • Mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail, na Publisher.

1.2.3 Ngazi ya Mshahara:

  • Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS C kwa Mwezi.

1.3 Dereva Vivuko Daraja la II – Nafasi 2

1.3.1 Kazi na Majukumu:

  1. Kufunga na kufungua kamba za mashua/kivuko.
  2. Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya mashua/vivuko.
  3. Kupanga abiria au magari kwenye mashua/vivuko.
  4. Kuendesha na kuongoza mashua/vivuko.
  5. Kutunza daftari za safari ya mashua/vivuko.
  6. Kuhakikisha injini za vivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
  7. Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.

1.3.2 Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha Nne.
  • Ujuzi wa kuendesha na kutunza mashua/vivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili.
  • Mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea, na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.

1.3.3 Ngazi ya Mshahara:

  • Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGOS A kwa Mwezi.

1.4 Dereva Daraja II – Nafasi 6

1.4.1 Kazi na Majukumu:

  1. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  2. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  3. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  4. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  5. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  6. Kufanya usafi wa gari.
  7. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

1.4.2 Sifa za Mwombaji:

  • Kidato cha Nne (Form IV).
  • Leseni ya Daraja E au C ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Mafunzo ya msingi ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.4.3 Ngazi ya Mshahara:

  • Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS B kwa Mwezi.

Masharti ya Jumla kwa Waombaji:

  1. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  3. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  4. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  5. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  6. Vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika vinapaswa kuambatanishwa. Shahada au Astashahada, Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificate, Vyeti vya kitaaluma pia vinatakiwa.
  7. “Testimonials,” “Provisional Results,” “Statement of results,” na hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  8. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  9. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  10. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 03 Septemba, 2024.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na nakala za vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, kwenda anuani ya:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino,
S.L.P 1126,
Dodoma.

Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mapendekezo:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.