Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Tabora 23-08-2024

Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Manispaa Ya Tabora 23-08-2024, Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kufuatia kibali hicho, Mkurugenzi anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:

1.0 DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)

1.1 Kazi na Majukumu

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi.
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari (log book).
  • Kufanya usafi wa gari.

1.1.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).
  • Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari, ambayo ameifanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.1.2 Ngazi ya Mshahara

  • Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali, yaani TGS B.

1.2 MTENDAJI WA MTAA III (NAFASI 05)

1.2.1 Majukumu ya Kazi

  • Kuwa Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa.
  • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao.
  • Kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Mtaa.
  • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji mipango ya maendeleo ya Mtaa.
  • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Mtaa.
  • Kutafsiri na kusimamia sera, sheria, na taratibu.
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
  • Kuongoza wakuu wa vitengo vya kitaaluma katika jamii.
  • Kusimamia, kukusanya, na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa.
  • Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Mtaa.
  • Kusimamia utungaji wa sheria ndogondogo za Mtaa.
  • Kupokea, kusikiliza, na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ndani ya Mtaa na kusoma mapato na matumizi kila baada ya miezi miwili.

1.2.2 Sifa za Kuajiriwa

  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).
  • Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

1.2.3 Ngazi ya Mshahara

  • Kwa kuzingatia ngazi za mshahara ya Serikali – TGS B.

1.3 MTENDAJI WA KIJIJI III (NAFASI 05)

1.3.1 Majukumu ya Kazi

  • Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
  • Katibu wa Kamati ya Kijiji.
  • Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Kijiji.
  • Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji.
  • Msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ndogo na Sheria nyingine zinazotumika katika Kijiji.
  • Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na umasikini katika Kijiji.
  • Kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi.

1.3.2 Sifa za Kuajiriwa

  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
  • Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo: Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

1.3.3 Ngazi ya Mshahara

  • Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 hadi 45 isipokuwa kwa wale walioko kazini Serikalini.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na kuainisha aina ya ulemavu walionao kwenye mfumo wa kuombea ajira.
  3. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV) yenye anuani, namba za simu zinazopatikana, na anuani ya barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
  4. “Provisional,” “Testimonials,” “Statement of results,” na hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita hazitakubaliwa.
  5. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  6. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  7. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti, wapitishe barua zao za maombi kupitia waajiri wao.
  8. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
  9. Waombaji waambatanishe vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili (Cheti cha Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, vyeti vya mafunzo mbalimbali).
  10. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika (TCU, NECTA, NACTVET).
  11. Uwasilishaji wa taarifa za kughushi utachukuliwa hatua za kisheria.
  12. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
  13. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 03 Septemba 2024.

MUHIMU:

Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Anuani ya barua iandikwe kwa:

Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Tabora,
Mtaa wa Ikulu,
Barabara ya Kiwanja cha Ndege,
S.L.P 174,
45182 TABORA.

Maombi yote ya kazi yatumwe kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu hayatafanyiwa kazi.

Imetolewa na:

MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI YA MANISPAA TABORA.

Soma Zaidi: Nafasi Za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chamwino 25-08-2024

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.