Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imepata kibali cha kutekeleza ajira mpya kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kibali hiki kinatoa nafasi kwa Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuomba nafasi mbalimbali zilizotangazwa.
Nafasi za Kazi Zinazopatikana
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba inatangaza nafasi za kazi zifuatazo:
1. Mtendaji wa Kijiji Daraja la III – Nafasi Tano (5)
Majukumu ya Kazi:
- Afisa Masuhuli na mtendaji mkuu wa serikali ya kijiji
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao
- Kuratibu na kusimamia mipango ya maendeleo ya kijiji
- Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
- Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi na kuhamasisha wananchi katika mipango ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji
- Mwenyekiti wa kikao cha wataalam waliopo katika kijiji
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
- Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
Sifa za Mwombaji:
- Elimu ya kidato cha nne au sita akiwa na Astashahada (NTA Level 5) katika moja ya fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa au chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara:
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS B.
2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi Mbili (2)
Majukumu ya Kazi:
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala kwenye rejista
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi kwenye rejista
- Kusambaza majalada kwa watendaji
- Kupokea majalada yanayorudi masijala toka kwa watendaji
- Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/majalada yanayohitajika na watendaji
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada au mahali pengine yanapohifadhiwa
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi
Sifa za Mwombaji:
- Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) akiwa na Stashahada (NTA level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
Mshahara:
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS C.
Masharti ya Jumla
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na anuani ya barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Julai, 2024.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; Recruitment Portal.
Hitimisho
Hii ni fursa muhimu kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika kujiunga na Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba. Kumbuka kufuata masharti yote yaliyoainishwa na kuwasilisha maombi yako kabla ya tarehe ya mwisho. Fursa hizi ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kitaalamu, hivyo usikose kuomba!
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya,
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba,
S.L.P 263,
Ifakara.
Soma Zaidi:
Tuachie Maoni Yako