Mfano wa barua ya kikazi TAMISEMI

Mfano wa barua ya kikazi TAMISEMI, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ni mojawapo ya taasisi muhimu nchini Tanzania inayohusika na utoaji wa ajira katika sekta mbalimbali za umma, ikiwemo ualimu na afya.

Kuandika barua ya maombi ya kazi ni hatua muhimu sana katika mchakato wa kutuma maombi ya ajira. Barua hii inahitaji kuandikwa kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha inatoa taarifa sahihi na yenye uwezo wa kumvutia mwajiri.

Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi

1. Kichwa cha Barua

  • Jina la mwombaji
  • Anwani ya mwombaji
  • Tarehe
  • Jina la mwajiri
  • Anwani ya mwajiri

2. Salamu

  • “Yah: Maombi ya Kazi ya Ualimu”

3. Utangulizi

  • Taja nafasi unayoomba na jinsi ulivyosikia kuhusu nafasi hiyo.

4. Kiini cha Barua

  • Eleza kwa kifupi kuhusu elimu yako na uzoefu wako wa kazi.
  • Taja sifa na ujuzi maalum unaomfanya uwe mgombea bora kwa nafasi hiyo.
  • Toa mifano ya mafanikio yako ya awali yanayohusiana na nafasi unayoomba.

5. Hitimisho

  • Eleza shauku yako ya kufanya kazi katika taasisi hiyo.
  • Toa shukrani kwa kuzingatia maombi yako.
  • Toa taarifa ya jinsi watakavyoweza kuwasiliana nawe.

6. Sahihi

  • Tumia neno la kufungia kama vile “Wako mtiifu,”
  • Sahihi yako
  • Jina lako kamili

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Ualimu TAMISEMI

Jina la Mwombaji Juma Hassan Mwambene
Anwani S.L.P 123, Dar es Salaam, Tanzania
Tarehe 07 Agosti 2024
Jina la Mwajiri Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, TAMISEMI
Anwani ya Mwajiri S.L.P 456, Dodoma, Tanzania

Yah: Maombi ya Kazi ya Ualimu

Ndugu Katibu,Napenda kuwasilisha maombi yangu ya kazi ya ualimu katika shule za serikali chini ya usimamizi wa TAMISEMI. Nimepata taarifa za nafasi hizi kupitia tovuti rasmi ya TAMISEMI.Nina shahada ya elimu (B.Ed) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na uzoefu wa miaka mitatu katika kufundisha masomo ya Sayansi katika shule za sekondari.

Katika kipindi chote cha kazi yangu, nimeweza kufanikisha ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi kwa asilimia 20 kupitia mbinu bora za ufundishaji na usimamizi wa darasa.

Nina ujuzi wa kutumia teknolojia katika ufundishaji, na pia nimekuwa nikishiriki katika programu za ziada za kuwawezesha wanafunzi kielimu na kijamii.

Sifa hizi, pamoja na uwezo wangu wa kufanya kazi kwa ushirikiano na walimu wenzangu, zinanifanya niwe mgombea bora kwa nafasi hii.Nina shauku kubwa ya kuchangia katika kuboresha elimu nchini kupitia nafasi hii ya ualimu.

Naamini kuwa kwa pamoja tunaweza kufanikisha malengo ya elimu ya taifa letu.Nashukuru kwa kuzingatia maombi yangu.

Tafadhali wasiliana nami kupitia namba ya simu 0712 345 678 au barua pepe juma.mwambene@example.com kwa maelezo zaidi.

Wako mtiifu,

Juma Hassan Mwambene

Mambo Muhimu ya Kuzingatia

  • Tumia majina yako kamili kama yanavyoonekana katika vyeti vya elimu.
  • Hakikisha barua yako ni fupi na ya moja kwa moja.
  • Tumia lugha rasmi na epuka makosa ya kisarufi.
  • Punguza mbwembwe wakati wa uandishi. Usiilembe barua kwa rangi au manjonjo ya aina yeyote. Kumbuka hii ni barua ya kazi na sio kadi ya mwaliko au barua inayotumwa kwa mpenzi wako.
  • Fuatilia maagizo yote yaliyotolewa kwenye tangazo husika la kazi.

Kwa kuzingatia muundo huu na mfano wa barua, utaweza kuandika barua ya maombi ya kazi inayokidhi vigezo na kumvutia mwajiri.

Mapendekezo:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.