Matokeo ya Simba Sc vs Dodoma Jiji Leo Septemba 29, 2024

Matokeo ya Simba Sc vs Dodoma Jiji Leo Septemba 29, 2024, Kwenye makala hii tunaangalia Matokeo ya Simba Dhidi ya Dodoma Jiji Leo Tarehe 29, 2024 Katika Uwanja wa Jamuhuri. 

Simba Sc vs Dodoma Jiji Leo Septemba 29, 2024

Leo usiku, macho yote yatakuwa kwenye dimba la Jamhuri Dodoma, ambapo Simba SC, maarufu kama “Mnyama,” itapambana na Dodoma Jiji kwenye mchezo wa nne wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.

Huu sio mchezo wa kawaida, ni zaidi ya vita ya alama tatu, ni kuendeleza rekodi safi ambayo Mnyama amekuwa nayo dhidi ya wapinzani hawa wa Dodoma.

Simba Leo terehe 29, septemba, 2024 Wameichapa Dodoma Jiji Goli 1 kwa sifuri Baada ya Kupata Mkwaju wa Penalti

Safari ya Ushindi ya Simba SC Dhidi ya Dodoma Jiji

Kwa kuanzia msimu wa 2020/2021, Simba SC imekuwa na rekodi ya kuvutia kila walipokutana na Dodoma Jiji. Hapa tunaangazia baadhi ya matukio muhimu yaliyopita:

Tarehe Uwanja Matokeo
Februari 4, 2021 Jamhuri, Dodoma Simba 2-1 Dodoma Jiji
Aprili 27, 2021 Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Simba 3-1 Dodoma Jiji
Oktoba 1, 2021 Jamhuri, Dodoma Simba 1-0 Dodoma Jiji
Machi 7, 2022 Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Simba 2-0 Dodoma Jiji
Oktoba 2, 2022 Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Simba 3-0 Dodoma Jiji
Januari 22, 2023 Jamhuri, Dodoma Simba 1-0 Dodoma Jiji
Agosti 20, 2023 Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Simba 2-0 Dodoma Jiji
Mei 17, 2024 Jamhuri, Dodoma Simba 1-0 Dodoma Jiji

Simba Imara, Dodoma Jiji Wakiwa na Presha

Kutazama takwimu hizi, inaonekana wazi kwamba Dodoma Jiji wamekuwa wakisumbuliwa mara kwa mara na Simba, iwe ugenini au nyumbani. Wakati Simba inakwenda Jamhuri leo, wenyeji wanajua kuwa kazi imekuwa ngumu zaidi ya kawaida.

Mara ya mwisho Simba kuondoka na ushindi wa 1-0 kwenye ardhi ya Dodoma, Mei 17, 2024, Mnyama alionyesha uwezo wake wa kucheza kwa nidhamu kubwa na kumiliki mpira.

Ni wazi kwamba wapinzani wao leo wanalenga kubadilisha matokeo, lakini Simba haina mpango wa kuruhusu mabadiliko haya kirahisi.

Je, Leo Itakuwaje?

Mchezo huu utapigwa majira ya saa 12:30 usiku, ambapo watazamaji wa Azam Sports 1 HD wataweza kufurahia mechi hii mubashara.

Wakati presha ya ushindi ikiwa juu kwa pande zote mbili, ni wazi kuwa Simba inataka kuendeleza wimbi la ushindi na kulinda nafasi yake katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Je, Dodoma Jiji watashindana na historia, au Simba ataendelea na utawala wake? Tunangojea kuona!

Mapendekezo:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.