Matokeo ya Kidato cha Sita 2024/2025 (Form Six Results), Matokeo ya Kidato cha Sita 2024/2025 ni matokeo ya mtihani wa mwisho wa Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari (ACSEE) uliofanyika mwezi Mei 2024. Mtihani huu ni muhimu kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Tanzania. Matokeo haya yanatumika kama kigezo na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kwa ajili ya udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu.
Tarehe za Kutolewa kwa Matokeo
Kwa kawaida, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hutangaza matokeo ya Kidato cha Sita ndani ya wiki mbili za kwanza za mwezi Julai kila mwaka. Hivyo, mwaka huu 2024, inatarajiwa kuwa matokeo yatatangazwa ndani ya kipindi hicho.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo
Wanafunzi na wazazi wanaweza kuangalia matokeo ya Kidato cha Sita kwa kufuata hatua zifuatazo:
Kupitia Tovuti ya NECTA:
-
- Tembelea tovuti ya NECTA: NECTA
- Chagua “Matokeo” kutoka kwenye menyu kuu.
- Chagua “ACSEE Results”.
- Bonyeza “ACSEE results 2024” ili kuona matokeo ya mwaka 2024.
- Tafuta jina la shule yako na bonyeza ili kuona matokeo ya shule hiyo.
Kupitia USSD:
-
- Piga *152*00#
- Chagua namba 8. ELIMU
- Chagua namba 2. NECTA
- Chagua aina ya mtihani 2. ACSEE
- Weka namba ya mtihani na mwaka, mfano: S0334-0556-2024
- Chagua aina ya malipo (gharama ya SMS ni Tshs 100/=)
- Utapokea ujumbe mfupi wenye matokeo yako.
Matokeo ya Kidato cha Sita 2024/2025 ni muhimu kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea na elimu ya juu. NECTA inatoa matokeo haya kupitia tovuti yao rasmi na njia ya USSD ili kurahisisha upatikanaji wake kwa wanafunzi na wazazi.
Mapendekezo:
Leave a Reply