Majina ya walioitwa kwenye usaili Jeshi la polisi 2024

Majina ya walioitwa kwenye usaili Jeshi la polisi 2024, (Waliochaguliwa Usail interview Jeshi La Polisi) Mkuu wa Jeshi la Polisi anapenda kuwatangazia kuwa vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Ajira TANZANIA POLICE FORCE RECRUITMENT PORTAL, usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 29/7/2024 hadi tarehe 11/8/2024 nchini kote.

Waombaji wa Tanzania Bara

  • Waombaji wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada: Usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) kilichopo Barabara ya Kilwa (Kurasini).
  • Waombaji wenye elimu ya Kidato cha Nne na Sita: Usaili wao utafanyika kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.

Waombaji wa Zanzibar

  • Waombaji wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Nne: Usaili utafanyika Zanzibar.
    • Kwa walioko Mikoa ya Unguja: Usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
    • Kwa walioko Mikoa ya Pemba: Usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).

Mahitaji Muhimu

Kila mmoja anatakiwa kufika akiwa na:

  • Vyeti halisi vya taaluma (academic certificates)
  • Cheti cha kuzaliwa
  • Kitambulisho cha Mamlaka ya Utambulisho wa Taifa (NIDA) au namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA)
  • Nguo na viatu vya michezo

Kijana yeyote atakayefika kwenye usaili baada ya tarehe 29/07/2024 hatopokelewa.

Orodha ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili imeambatishwa pamoja na tangazo hili.

Imewasilishwa na:

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Makao Makuu ya Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA 22/07/2024

PDF Majina Yote Hapa (TANGAZO-LA-KUITWA-KWENYE-USAILI-JULY-2024.pdf)

Maelezo Zaidi Kuhusu Usaili wa Ajira ya Jeshi la Polisi

Ndugu vijana wa Tanzania, fursa ya kujiunga na Jeshi la Polisi ni muhimu na yenye thamani kwa ustawi wa nchi yetu. Kupitia ajira hii, mnapata nafasi ya kuhudumia taifa kwa moyo wa uzalendo na kujituma.

Katika hatua hii muhimu ya usaili, ni vyema kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha mnafanikiwa na kuwa sehemu ya kikosi hiki muhimu cha usalama wa nchi.

Kwa wale waliochaguliwa, hakikisheni mnaandaa vyeti vyenu halisi na dokumenti zingine zote zinazohitajika. Hii itasaidia kurahisisha mchakato wa usaili na kuepusha usumbufu usio wa lazima.

Pia, kumbukeni kujiandaa kisaikolojia na kimwili kwa usaili huu kwa kufanya mazoezi na kujitayarisha kiakili.

Tunawatakia kila la heri katika usaili wenu na tunategemea kuwaona mkiwa sehemu ya Jeshi la Polisi Tanzania, mkifanya kazi kwa uaminifu, bidii, na uzalendo. Fursa hii ni hatua moja mbele katika kuboresha maisha yenu na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa katika usalama na maendeleo ya nchi yetu.

Soma Zaidi:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.