Madaraja ya Mserereko 2024/2025

Madaraja ya Mserereko 2024/2025, Kwa mwaka wa fedha 2024/2025, serikali ya Tanzania imepanga kupandisha madaraja walimu 54,000 ambao walikuwa waliachwa nyuma kimadaraja. Hatua hii inalenga kuleta usawa katika madaraja kwa kuzingatia kiwango cha elimu na muda wa ajira wa walimu hao.

Kupanda Madaraja

Ili mwalimu aweze kupanda daraja, ni lazima akidhi vigezo vilivyowekwa na serikali, ambavyo ni pamoja na:

  • Uwepo wa Muundo wa Kada ya Mwalimu: Mwalimu anapaswa kuwa katika muundo rasmi wa kada.
  • Uwepo wa Bajeti ya Mishahara: Bajeti ya mishahara na ikama lazima iwe imeidhinishwa.
  • Kuthibitishwa Kazini: Mwalimu anayepandishwa cheo lazima awe amethibitishwa kazini.
  • Utendaji Kazi Mzuri: Mwalimu lazima awe na utendaji kazi mzuri uliopimwa kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu kupitia Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS).
  • Uzoefu wa Kutosha: Awe na uzoefu wa kutosha katika cheo anachokitumikia.

Serikali imekuwa ikifanya juhudi za kutatua changamoto zinazowakabili walimu, kama vile ucheleweshaji wa upandishwaji wa madaraja na malimbikizo ya mishahara.

Dkt. Charles Msonde, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI, alieleza kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango wa kupandisha madaraja walimu ili kuboresha mazingira yao ya kazi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu upandishwaji wa madaraja ya walimu na masuala mengine yanayohusiana na ajira za walimu, unaweza kutembelea:

Tovuti ya TAMISEMI kwa taarifa za serikali kuhusu masuala ya walimu.

Jamii Forums kwa mijadala na maoni ya walimu kuhusu upandishwaji wa madaraja.

Mpango huu wa kupandisha madaraja unalenga kuboresha hali ya walimu na kuongeza motisha yao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Mapendekezo:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.