Ku- confirm Mwajiri ajira Portal (Kada ya Elimu N.K)

Jinsi ya Ku- confirm Mwajiri ajira Portal (Kada ya Elimu N.K),  Ajira Ualimu utumishi Angalieni status zenu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, inapenda kuwajulisha wale wote walioomba kazi ya kufundisha katika Mikoa tofauti tofauti kuwa, imetoa siku tatu kuanzia terehe 14 mpaka16 Septemba, 2024 kwa ajili ya kuhuisha (update) taarifa zao za Mkoa ulioomba kufanya kazi katika mfumo wa Ajira Portal endapo unasomeka tofauti na Mkoa ambao ungependa kufanya kazi.

Aidha, Hakikisha Mkoa unaosomeka katika eneo la Mwajiri “Employer” ndilo ulilo omba kama ni tofauti unapaswa kubadilisha kwenye mfumo kwani sehemu hii ndio itakayopelekea kupangiwa kituo cha Usaili wa Mahojiano na hatimaye kupangiwa kituo cha kazi.

Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni sikivu, imesikia maombi yenu hivyo, imetoa siku tatu tu kwa ajili ya kuhuisha taarifa zenu. Changamoto hii imejitokeza wakati wa kutuma maombi ya kazi ambapo waombaji wengi walijaziwa taarifa zao na ndugu, jamaa na hata wahudumu wa ‘stationaries’ na hamkupata nafasi ya kuhakiki kilichojazwa kama ni sahihi.

Kutokana na changamoto hiyo, ofisi inawasisitiza watafuta fursa za ajira kuwa makini wakati wote wa ujazaji wa taarifa katika mfumo wa Ajira Portal na kuhakiki taarifa zao ili kuepuka usumbufu.

Ili kuweza kufanikisha kuhuisha taarifa zako katika mfumo wa Ajira Portal fuata maelekezo yafuatayo;

  1. Ingia katika akaunti yako ya Ajira Portal;

 

  1. Nenda Sehemu iliyoandikwa “My APPLICATIONS” kwenye Akaunti yako ya Ajira Portal kisha bonyeza sehemu hiyo;

  1. Chagua Sehemu iliyoandikwa “SELECT EMPLOYER” kisha bonyeza hapo na kuchagua mkoa ambao ungependa kufanya kazi;

 

 

  1. Kisha ujumbe utakuja “CONFIRM EMPLOYER” wa kukutaka Uthibitishe Mwajiri “Employer” kwa Maana ya mkoa uliochagua kuwa ni sahihi na itakulazimu ubonyeze sehemu iliyoandikwa SUBMIT kwa ajili ya kuwasilisha;

  1. Kisha utaona ujumbe umeandikwa “EMPLOYER CONFIRMED SUCCESSFULLY”. Hii itamaanisha kuwa umefanikiwa kubadilisha/kuhuisha na kuchagua mkoa ambao ungependa kufanya

Ukimaliza ukienda katika Akaunti yako utaweza kuona mkoa ulio chagua na mkoa huo ndio utapelekea kupangiwa kituo cha kazi baada ya kufaulu usaili wa mahojiano.

Vile vile waomba kazi wanatakiwa kuhuisha taarifa zao katika sehemu ya “Current address” sehemu iliyoandikwa “current resident region” na “current resident district” taarifa zinazo onekana sehemu hii ndizo zitakazo tumika kupanga sehemu ya kufanyia usaili wa Kuandika/Mchujo (Aptitude Test)

Mapendekezo:

Nini Kipya Huku ajira portal (walimu)

Ajira Portal Login (Mfumo wa Maombi ya ajira) 

Walioitwa kwenye interview Utumishi 2024 (Usaili) Ajira Portal

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa umma itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na vilevile kusikiliza na kuyafanyia kazi maoni mbalimbali yanayotolewa na wadau kwa lengo la kuboresha zaidi mchakato wa ajira.

Lynn Chawala

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.