Jinsi ya kupata kitambulisho cha NIDA

Jinsi ya kupata kitambulisho cha NIDA, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) nchini Tanzania inatoa vitambulisho vya aina tatu: Kitambulisho cha Raia, Kitambulisho cha Mgeni Mkazi, na Kitambulisho cha Mkimbizi. Kitambulisho cha NIDA ni muhimu kwa utambulisho rasmi na kupata huduma mbalimbali nchini.

Hapa chini ni mwongozo wa jinsi ya kupata kitambulisho hiki.

Mahitaji ya Kitambulisho cha Raia

Ili kupata Kitambulisho cha Raia, unahitaji nyaraka zifuatazo:

  • Cheti cha kuzaliwa
  • Cheti cha elimu ya msingi na sekondari (kidato cha IV na VI)
  • Pasi ya kusafiria (Pasipoti)
  • Leseni ya udereva
  • Kadi ya bima ya afya
  • Kadi ya mfuko wa hifadhi ya jamii
  • Kadi ya mpiga kura
  • Nambari ya mlipa kodi (TIN)
  • Kitambulisho cha mzanzibar mkazi
  • Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa.

Mahitaji ya Kitambulisho cha Mgeni Mkazi

Kwa mgeni mkazi, mahitaji ni:

  • Pasipoti ya nchi anakotoka
  • Kibali cha kukaa nchini na kufanya shughuli mbalimbali.

Mahitaji ya Kitambulisho cha Mkimbizi

Kwa mkimbizi, unahitaji:

  • Hati inayothibitisha hadhi ya mkimbizi nchini.

Hatua za Kupata Kitambulisho

Jaza Fomu ya Maombi: Tembelea mfumo wa maombi ya NIDA na ujaze fomu ya maombi ya kitambulisho kwa njia ya kielektroniki. Hakikisha unachapisha fomu hiyo baada ya kujaza.

Wasilisha Fomu na Nyaraka: Peleka fomu iliyojazwa pamoja na nyaraka zinazohitajika katika ofisi ya NIDA ya wilaya iliyo karibu nawe. Hapa, utasajili alama za kibaiolojia.

Thibitisha Maombi Yako: Baada ya kuwasilisha maombi, unaweza kufuatilia hali ya kitambulisho chako kupitia mfumo wa NIDA ili kujua kitambulisho chako kipo wapi.

Mahitaji

Aina ya Kitambulisho Mahitaji
Kitambulisho cha Raia Cheti cha kuzaliwa, cheti za elimu, pasi ya kusafiria, leseni ya udereva, kadi ya bima, n.k.
Kitambulisho cha Mgeni Mkazi Pasipoti ya nchi anakotoka, kibali cha kukaa nchini
Kitambulisho cha Mkimbizi Hati ya mkimbizi

Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti ya NIDA kwa mwongozo wa kina.

Mapendekezo:

 

Nimebobea kwenye uandaaji wa makala za mtandaoni, Makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.