Jinsi ya kulipa ada CCM

Jinsi ya kulipa ada CCM, Ada za Uanachama wa CCM, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka mfumo rahisi wa kulipia ada za uanachama ili kuwezesha wanachama wake kufanya malipo kwa urahisi.

Ada hizi zinaweza kulipwa kupitia njia mbalimbali za kielektroniki kama vile T-PESA, M-PESA, Tigo Pesa, Airtel Money, na SimBanking ya CRDB. Hapa chini ni maelezo ya jinsi ya kulipia ada za uanachama wa CCM.

Njia za Kulipia Ada

T-PESA

  1. Piga *150*71#.
  2. Chagua 5 ‘Huduma za kifedha’.
  3. Chagua 1 ‘TTCL Kwenda Benki’.
  4. Chagua 2 ‘Orodha ya Benki’.
  5. Chagua 2 ‘CRDB’.
  6. Ingiza namba ya malipo (Mfano: C0000000102301).
  7. Weka kiasi.
  8. Weka namba ya siri.

M-PESA

  1. Piga *150*00#.
  2. Chagua 6 ‘Huduma za kifedha’.
  3. Chagua 2 ‘Mpesa kwenda Benki’.
  4. Chagua 1 ‘Kwenda CRDB’.
  5. Chagua 2 ‘Weka Control Number’.
  6. Ingiza namba yako ya Kielektroniki (Mfano: C0000000102301).
  7. Weka kiasi.
  8. Weka namba yako ya siri.
  9. Chagua 1 ‘Kubali’.

Tigo Pesa

  1. Piga *150*01#.
  2. Chagua 4 ‘Lipa Bili’.
  3. Chagua 3 ‘Ingiza Namba ya kampuni’.
  4. Namba ya Kampuni ni 900600.
  5. Weka Kumbukumbu Namba [Namba yako ya kielektroniki, Mfano: C0000000102301].
  6. Weka kiasi.
  7. Weka Namba ya Siri.
  8. Chagua 1 ‘Kubali’.

Airtel Money

  1. Piga *150*60#.
  2. Chagua 1 ‘Tuma Pesa’.
  3. Chagua 4 ‘Tuma Kwenda Benki’.
  4. Chagua 2 ‘CRDB’.
  5. Chagua 2 ‘Lipa kwa Namba ya Malipo’.
  6. Ingiza namba ya Kumbukumbu.
  7. Weka namba yako ya kielektroniki (Mfano: C0000000102301).
  8. Weka kiasi cha Pesa.
  9. Weka neno la siri.

CRDB Bank (SimBanking)

  1. Malipo.
  2. Malipo Zaidi.
  3. CCM Payment.
  4. Ingiza Namba ya Malipo (Mfano: C0000000102301).
  5. Pata Taarifa.
  6. Weka Kiasi.
  7. Endelea.
  8. Thibitisha.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kulipia ada za uanachama wa CCM, unaweza kutembelea tovuti ya CCM Mwanachama.

Mfumo huu wa malipo unalenga kurahisisha mchakato wa kulipia ada na kuhakikisha kuwa wanachama wanapata huduma bora na kwa wakati.

Nimebobea kwenye uandaaji wa makala za mtandaoni, Makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.