Jinsi ya Kubadili Kituo Cha Usaili Ajira Portal, Mkoa (ajira Za Walimu au Ualimu) Umeomba kazi ya ualimu lakini unataka kubadili kituo cha usaili kupitia Ajira Portal? Usiwe na shaka, makala hii itakuongoza hatua kwa hatua jinsi ya kufanya mabadiliko hayo kwa urahisi.
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetambua changamoto zinazowakumba waombaji wa kazi na imeamua kutoa fursa ya siku tatu ili kuhuisha taarifa zako.
Hatua za Kufuatilia
Kwanza kabisa, ni muhimu kufuata hatua hizi ili kubadilisha kituo chako cha usaili:
Ingia Kwenye Akaunti Yako ya Ajira Portal
Tumia kifaa chako cha kielektroniki kuingia kwenye mfumo wa Ajira Portal kupitia tovuti rasmi Ajira Portal.
Nenda kwenye Sehemu ya “My Applications”
Baada ya kuingia, fungua sehemu ya My Applications inayopatikana kwenye akaunti yako ya Ajira Portal.
Chagua Sehemu ya “Select Employer”
Hapa utaona sehemu ya kuchagua mwajiri. Bonyeza hapo na kisha chagua mkoa ambao ungependa kufanya kazi.
Thibitisha Uchaguzi wa Mkoa
Baada ya kuchagua mkoa, ujumbe utaonekana ukiomba uthibitishe kama mkoa uliouchagua ni sahihi. Thibitisha kwa kubonyeza Submit.
Ujumbe wa Mafanikio
Utaona ujumbe ukisema “Employer Confirmed Successfully,” ambao utathibitisha kuwa umefanikiwa kubadilisha kituo cha usaili.
Muhimu Zaidi!
Tafadhali hakikisha umehuisha taarifa zako kwenye sehemu ya anwani ya sasa (Current Resident Region na Current Resident District). Hii ni muhimu kwani taarifa hizi ndizo zitakazotumika kukupangia sehemu ya kufanyia usaili wa kuandika au mchujo (Aptitude Test).
Kwa wale ambao walikosea kujaza taarifa zao wakati wa awali, Sekretarieti ya Ajira imeelewa changamoto hizo, hasa kwa wale waliotumia watu wengine kuwasaidia kuomba kazi. Fursa hii ni ya kipekee, hivyo hakikisha umehakiki taarifa zako kwa umakini ili kuepuka usumbufu wa baadaye.
Mapendekezo:
Ku- confirm Mwajiri ajira Portal (Kada ya Elimu N.K)
Nini Kipya Huku ajira portal (walimu)
Ajira Portal Login (Mfumo wa Maombi ya ajira)
Kubadilisha kituo cha usaili kupitia Ajira Portal ni rahisi ikiwa utafuata hatua hizi. Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inaendelea kuboresha mchakato wa ajira kwa kuhakikisha kila mwombaji anapata taarifa sahihi na huduma bora.
Tuachie Maoni Yako