Huduma Kwa Wateja Nida; Mawasiliano yao Namba za simu

Huduma Kwa Wateja Nida; Mawasiliano yao Namba za simu,  Wazo la kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilizaliwa mwaka 1968 katika kikao cha “Interstate Intelligence Gathering” kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia.

Kwa wakati huo nchi za Kenya na Zambia tayari zilikuwa na Vitambulisho vyao vya Taifa. Iliazimiwa kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria katika nchi hizo nne ni lazima nchi za Uganda na Tanzania nazo zikatoa Vitambulisho vya Taifa kwa raia wao.

Kumekuwa na jitihada mbalimbali za Serikali kuhakikisha Watanzania na wageni wakazi wote wanapatiwa Vitambulisho vya Taifa, lakini jitihada hizo hazikuweza kuzaa matunda yaliyotajariwa kwa kipindi kirefu kutokana na sababu mbalimbali. Mwaka 1986 Serikali ilitunga Sheria ya Vitambulisho ambayo haikutumika wala kutungiwa kanuni zake.

Ni wazi kwamba kwa wakati huu kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na Vitambulisho vya Taifa kulingana na mazingira yaliyopo. Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo nchi tano zimeungana na kukubaliana kwamba watu wa nchi hizo wanaweza kutembeleana bila bughudha pia kumeongeza umuhimu wa kuwa na Vitambulisho. Ikumbukwe kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee katika Jumuiya hiyo ambayo haina Vitambulisho vya Taifa.

Huduma Kwa Wateja Nida

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.