Gharama za vifurushi vya bima ya afya NHIF 2024

Gharama za vifurushi vya bima ya afya NHIF 2024 Bei Zote Hapa, Bima ya afya ni muhimu kwa kila mtu, hasa katika nyakati hizi ambapo gharama za matibabu zimepanda.

Katika Tanzania, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hutoa vifurushi mbalimbali vya bima ya afya kwa mwaka 2024. Hapa tutazungumzia gharama za bima ya afya kwa makundi tofauti ya watu na umuhimu wake.

Gharama za Vifurushi vya Bima ya Afya (NHIF) 2024

Kundi la Umri: Miaka 18 hadi 35

  1. I Care Health – Shilingi 192,000
  2. Invest Health – Shilingi 384,000
  3. Fulfill Health – Shilingi 516,000

Kundi la Umri: Miaka 39 hadi 59

  1. I Care for Health – Shilingi 240,000
  2. Invest in Health – Shilingi 440,000
  3. Fulfill Health – Shilingi 612,000

Kundi la Umri: Miaka 60 na Zaidi

  1. I Care for Health – Shilingi 336,000
  2. Invest in Health – Shilingi 660,000
  3. Fulfill Health – Shilingi 984,000

Maono ya NHIF

NHIF inalenga kuwa programu bora ya bima ya afya katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Dhamira ya NHIF

NHIF imejidhatiti kutoa huduma bora za bima ya afya kwa wanachama wake ili waweze kupata huduma za matibabu kupitia mtandao mpana wa vituo vya afya vilivyoidhinishwa.

Misingi ya NHIF

NHIF inathamini na kuzingatia maadili yafuatayo:

  • Uadilifu
  • Uwajibikaji
  • Ubunifu
  • Ukarimu
  • Kasi
  • Kujali

Umuhimu wa Bima ya Afya

Bima ya afya ni muhimu kwani gharama za matibabu zimekuwa juu sana. Kwa mfano, gharama za matibabu ya saratani kwa mwaka mmoja zimefikia shilingi milioni 69.9, matibabu ya figo shilingi milioni 35, na upasuaji wa moyo shilingi milioni 12. Hizi gharama ni kubwa mno kwa mwananchi wa kawaida kuweza kumudu bila bima ya afya.

Soma Zaidi:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.