Kurefusha na Kukuza Nywele
Mafuta ya mnyonyo yana asidi za omega-6 na omega-9 ambazo ni virutubisho muhimu kwa afya ya nywele. Hizi asidi husaidia kukuza nywele na kuzirefusha kwa haraka. Ukitumia mafuta ya mnyonyo mara kwa mara, unaweza kuona ongezeko la urefu wa nywele na kupunguza kasi ya kunyolewa kwa nywele.
Kutibu Mba na Matatizo ya Ngozi ya Kichwa
Mafuta ya mnyonyo yana uwezo wa kuua bacteria na fangasi ambao huweza kusababisha matatizo kama mba kichwani. Ukichanganya mafuta ya mnyonyo na mafuta ya mzeituni na kupaka kichwani, itasaidia kutibu mba na kurudisha afya ya nywele.
Kuondoa Michirizi na Makovu
Mafuta ya mnyonyo yana uwezo wa kuondoa michirizi na makovu kwenye ngozi ya kichwa. Hii husaidia kurudisha afya ya nywele na kuongeza ukuaji.
Kutibu Chunusi
Mafuta ya mnyonyo yana kiungo kinachoua bacteria wanaosababisha chunusi. Ukipaka usoni, itasaidia kutibu na kuzuia chunusi.
Kutibu Matatizo ya Hedhi
Inasemekana mafuta ya mnyonyo yamekuwa na mafanikio pia katika kutibu matatizo mbalimbali ya hedhi kwa wanawake.
Kusaidia Uzazi
- Faida za mafuta ya mnyonyo kwenye nywele
- Jinsi Ya Kupunguza Tumbo Kwa Kutumia Mafuta Ya Nyonyo
- Faida za mafuta ya mnyonyo kwenye ngozi
- Jinsi Ya Kutengeneza Mafuta Ya Mnyonyo
Tuachie Maoni Yako