Droo ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Wanawake CAF 2024, kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Wanawake wa CAF itafanyika Julai 24, mwaka huu. Michuano hii ni muhimu kwa timu zinazoshiriki, kwani itatoa fursa kwa klabu bora kuweza kuwakilisha nchi zao katika mashindano ya kimataifa. Hapa chini ni orodha ya timu zilizoingizwa kwa kanda tofauti pamoja na tarehe za mashindano ya kufuzu.
WAFU B (10 – 23 Agosti)
- Ainonvi FC (Benin)
- Hasaacas Ladies (Ghana)
- Inter d’Abidjan (Côte d’Ivoire)
- AO Étincelles OU USFA (Burkina Faso)
- AS Garde Nationale (Niger)
- Edo Queens (Nigeria)
- ASKO de Kara (Togo)
UNAF (21 – 31 Agosti)
- CF Akbou (Algeria)
- Tutankhamun (Misri)
- AS Far (Morocco)
- ASF Sousse (Tunisia)
CECAFA (17 Agosti – 4 Septemba)
- PVP Buyenzi (Burundi)
- FAD (Djibouti)
- CBE FC (Ethiopia)
- Kenya Police Bullets (Kenya)
- Kawempe Muslim (Uganda)
- Rayon Sports (Rwanda)
- Yei Joint Stars (Sudan Kusini)
- Simba Queens (Tanzania)
- Warriors Queens (Zanzibar)
UNIFFAC (16 – 24 Agosti)
- Lekié FF (Cameroon)
- TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)
- Atlético de Malabo (Equatorial Guinea)
- CSM Diables Noirs (Congo)
Matarajio ya Mashindano
Mashindano haya yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali, kwani timu nyingi zina nia ya kutwaa ubingwa na kuwakilisha nchi zao kwenye Ligi ya Mabingwa Wanawake wa CAF. Wakati droo itakapofanyika, mashabiki wataweza kuona jinsi timu zao zitakavyojiandaa kwa michuano hii mikubwa.
Tunatarajia kuona michezo mizuri na wachezaji wakitoa kiwango cha juu ili kuweza kufuzu katika mashindano haya. Huu ni wakati mzuri kwa soka la wanawake barani Afrika, na ni matumaini yetu kuwa timu zitaonesha uwezo wao na kufanya vizuri kwenye uwanja.
Tuwape sapoti wachezaji wetu na timu zinazoshiriki, huku tukisubiri kwa hamu kuona matokeo ya droo hii na jinsi itakavyoshirikisha timu zetu kwenye Ligi ya Mabingwa Wanawake wa CAF!
Soma Zaidi:
Tuachie Maoni Yako