Call forwarding ni huduma ya simu inayoruhusu mpigaji kuelekeza simu inayoingia kwa nambari nyingine ya simu. Badala ya simu kupokelewa moja kwa moja kwenye nambari iliyoitiwa, inapelekwa kwa nambari tofauti ambayo mpigaji ameweka.
Huduma hii hutumika wakati unataka simu zako ziende kwa nambari nyingine, kwa mfano, ikiwa uko mbali na simu yako, uko busy, au simu yako haipatikani.
Aina za call forwarding ni kama zifuatazo:
Forwarding wakati namba yako haipatikani – Simu itaelekezwa ikiwa huna network.
Forwarding wakati uko kwenye simu nyingine – Inasaidia ikiwa tayari uko kwenye simu nyingine na hutaki kupoteza simu inayoingia.
Forwarding wakati hujibu simu – Ikiwa haufikiwi baada ya muda fulani, simu itaelekezwa kwa nambari nyingine.
Forwarding mara zote – Simu zote zinazoingia zinaelekezwa moja kwa moja kwa nambari nyingine bila kupigiwa kwanza.
Hii ni muhimu kwa watu wanaotaka kuhakikisha hawakosi simu muhimu wanapokuwa hawapatikani.
Tuachie Maoni Yako