Serikali za mitaa nchini Tanzania zilianza kuanzishwa rasmi mwaka 1982. Hii ilikuwa ni baada ya kutolewa kwa sheria mbalimbali ambazo ziliweka misingi ya mfumo wa serikali za mitaa, ikiwemo Sheria Na. 7 ya Halmashauri za Wilaya na Sheria Na. 8 ya Halmashauri za Miji, zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya mwaka 1982, mfumo wa serikali za mitaa ulipitia mabadiliko kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa halmashauri za wilaya mwaka 1972 na kuanzishwa kwa mfumo wa madaraka mikoani, ambao ulilenga kuhamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi.
Hata hivyo, kutokana na changamoto zilizojitokeza katika mfumo huo, serikali iliona umuhimu wa kurejesha mamlaka za serikali za mitaa ili kuwezesha wananchi kujiamulia mambo yao wenyewe.
Mwaka 1984, utekelezaji wa mfumo huu wa serikali za mitaa ulianza rasmi, ukilenga kuimarisha demokrasia shirikishi na kuwapa wananchi mamlaka zaidi katika ngazi za chini za utawala
Tuachie Maoni Yako