Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Hufanyika Mwezi Wa Ngapi?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa, alitangaza rasmi tarehe hiyo mnamo Agosti 15, 2024. Uchaguzi huu utahusisha uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa halmashauri za vijiji, wenyeviti wa mitaa, na wajumbe wa kamati za mitaa.

Ratiba ya Uchaguzi:

Uandikishaji wa wapiga kura: Utakuwa kati ya Oktoba 11 hadi 20, 2024.

Uteuzi wa wagombea: Utafanyika tarehe Novemba 8, 2024.

Kampeni: Zitaanza tarehe Novemba 20 na kumalizika Novemba 26, 2024.

Upigaji kura: Utanza saa mbili asubuhi na kumalizika saa kumi jioni.

Waziri Mchengerwa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika uchaguzi huu muhimu kwa kujiandikisha na kupiga kura.

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.