Forbes imetangaza orodha ya mabilionea wa Afrika kwa mwaka 2024, ambapo jumla ya mabilionea 20 wana thamani ya dola bilioni 82.4, ongezeko la dola milioni 900 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Hapa kuna orodha ya matajiri kumi bora:
Nafasi | Jina | Utajiri (TZS trilioni) |
---|---|---|
1 | Aliko Dangote | 34.8 |
2 | Johann Rupert na familia | 25.3 |
3 | Nicky Oppenheimer na familia | 23.5 |
4 | Nassef Sawiris | 21.8 |
5 | Mike Adenuga | 17.3 |
6 | Abdulsamad Rabiu | 14.7 |
7 | Naguib Sawiris | 9.5 |
8 | Mohamed Mansour | 8 |
9 | Koos Bekker | 6.7 |
10 | Patrice Motsepe | 6.7 |
Mohammed Dewji, mjasiriamali wa Tanzania, amepanda kutoka nafasi ya 15 hadi nafasi ya 12, akiwa na utajiri wa TZS trilioni 4.5.
Orodha hii inaonyesha mabadiliko katika utajiri wa matajiri wa Afrika na inatoa picha ya maendeleo na changamoto zinazokabili sekta za biashara barani humo
Tuachie Maoni Yako