Ratiba ya Mtihani Darasa la Saba (7) 2024/2025 NECTA

Ratiba ya Mtihani Darasa la Saba (7) 2024/2025 NECTA PDF Ratiba darasa la saba 2024 exam timetable, Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) ni kipimo muhimu kwa wanafunzi wote nchini Tanzania. Mtihani huu huandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) na unafanyika kila mwaka mwezi Septemba.

Mwaka huu, mtihani huu utafanyika tarehe 11 na 12 Septemba, 2024. Hapa chini ni ratiba ya mtihani pamoja na maelekezo muhimu kwa watahiniwa.

Ratiba ya Mtihani

Jumatano, 11 Septemba 2024

  • 2:00 – 3:40: Kiingereza (English Language)
  • 3:40 – 4:30: Mapumziko
  • 4:30 – 6:00: Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi (Social Studies and Vocational Skills)
  • 6:00 – 8:00: Mapumziko
  • 8:00 – 9:30: Sayansi na Teknolojia (Science and Technology)

Alhamisi, 12 Septemba 2024

  • 2:00 – 4:00: Hisabati (Mathematics)
  • 4:00 – 5:00: Mapumziko
  • 5:00 – 6:40: Kiswahili
  • 6:40 – 8:30: Mapumziko
  • 8:30 – 10:00: Uraia na Maadili (Civic and Moral Education)

Maelekezo Muhimu kwa Watahiniwa

  1. Ratiba ya Mtihani: Hakikisha unayo ratiba ya mtihani iliyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
  2. Uhakiki wa Somo: Soma jina la somo juu ya bahasha husika na thibitisha kuwa ndilo somo linalostahili kufanyika wakati huo.
  3. Sauti ya Mtahiniwa: Kabla ya kufungua bahasha, mpe mtahiniwa asome kwa sauti jina la somo lililoandikwa juu ya bahasha ili kuthibitisha ni somo sahihi.
  4. Utata wa Maelekezo: Endapo kuna utata kati ya maelekezo yaliyomo kwenye karatasi ya mtihani na ratiba ya mtihani, fuata maelekezo yaliyomo kwenye karatasi ya mtihani.
  5. Mahitaji Maalum: Watahiniwa wenye mahitaji maalum (wasioona, uoni hafifu, viziwi) waongezewe muda wa ziada wa dakika 20 kwa kila saa kwa somo la Hisabati na dakika 10 kwa kila saa kwa masomo mengine.
  6. Karatasi za Mtihani: Watahiniwa wenye uoni hafifu wapewe karatasi za mtihani zenye maandishi yaliyokuzwa zilizoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
  7. Maelekezo ya Jumla:
    • Watahiniwa waingie ndani ya chumba cha mtihani nusu saa kabla ya muda wa mtihani.
    • Wanaochelewa kwa zaidi ya nusu saa baada ya mtihani kuanza hawataruhusiwa kuingia.
    • Fuata maelekezo yote yatakayotolewa na wasimamizi wa mtihani.
    • Andika namba ya mtihani kwa usahihi.
    • Usifanye mawasiliano ya maneno au kwa njia yoyote baina ya watahiniwa. Ikiwa mtahiniwa ana tatizo, inapaswa kunyoosha mkono ili kuomba msaada kwa msimamizi wa mtihani.
    • Kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaojihusisha matokeo yao yatafutwa.

Kufanya mtihani ni sehemu muhimu ya safari ya elimu ya mwanafunzi. Ni muhimu kwa watahiniwa kufuata ratiba na maelekezo yaliyotolewa ili kuhakikisha mtihani unafanyika kwa haki na usawa. Tunawatakia watahiniwa wote kila la heri katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi wa mwaka 2024.

PDF Hapa; https://necta.go.tz/files/PSLE_TIMETABLE_2024.pdf

Soma Zaidi:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.