Vyakula Bora Vya Kula Kabla Ya Tendo La Ndoa

Vyakula Bora Vya Kula Kabla Ya Tendo La Ndoa, Kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vimeonekana kuwa na uwezo wa kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa na kuboresha utendaji wake. Haya ni vyakula ambavyo vina vitamini, madini na kemikali mbalimbali zinazohitajika katika mfumo wa uzazi na kuongeza msisimko wa kimapenzi.Baadhi ya vyakula hivi ni pamoja na:

1. Pilipili

Pilipili zina kinachojulikana kama capsaicin, ambayo utafiti umebaini inaweza kuchochea homoni ya endorphins (ya kujihisi furaha) na kusisimua mfumo wa fahamu. Pia pilipili husaidia kuboresha mzunguko wa damu, hali inayohitajika katika kuongeza msisimko wa kimapenzi na utendaji bora wa tendo la ndoa.

2. Matunda na Mboga za Majani

Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol). Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.

Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.

3. Nafaka Zisizokobolewa

Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu.

Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo. Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

4. Tangawizi

Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu. Tangawizi pia ina uwezo wa kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na kuboresha utendaji wa tendo la ndoa.

5. Asali

Asali ina madini ya boron ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume. Pia asali husaidia katika kuongeza mzunguko wa damu na kutoa hisia nzuri za kujamiiana.

6. Karanga

Karanga zina protini nyingi ambazo husaidia katika kuongeza nguvu na uimara wa mwili wakati wa tendo la ndoa. Pia karanga zina L-arginine ambayo husaidia katika kuongeza mzunguko wa damu kwenye uume.

7. Chaza (Oysters) na Pweza

Chaza na pweza zina zinc kwa wingi ambazo husaidia katika uzalishaji wa homoni za kiume na kuboresha utendaji wa tendo la ndoa. Pia zinc husaidia katika kuongeza idadi na ubora wa mbegu za kiume.

8. Soya

Soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada. Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

9. Chokoleti

Chokoleti ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chokoleti masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.

10. Parachichi

Parachichi linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

Mapendekezo:

Kwa ujumla, kula vyakula hivi vya asili kwa kiasi cha kutosha kabla ya tendo la ndoa kunaweza kuongeza hamu na utendaji bora wa tendo. Lakini pia ni muhimu kuzingatia masuala mengine kama afya ya mwili, hali ya akili na mawasiliano bora katika uhusiano ili tendo la ndoa liweze kuwa la kuridhisha kwa wote.

Nimebobea kwenye uandaaji wa makala za mtandaoni, Makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.