Je, Kutoa Pesa Payoneer Kuja Bank nitumie NMB au CRDB?

Je, Kutoa Pesa Payoneer Kuja Bank nitumie NMB au CRDB?, Kutoa pesa kutoka Payoneer kuja benki ni moja ya njia zinazowapa changamoto watu wengi. Hata hivyo, unapotumia NMB au CRDB, zote zinawezekana. Mchakato mzima unategemea usahihi wa maelezo unayoweka, hususani SWIFT Code na namba yako ya akaunti. SWIFT Code za benki kuu hizi mbili ni kama ifuatavyo:

  • CRDB – CORUTZTZXXX
  • NMB – NMIBTZTZXXX

Garama za SWIFT Transfer

Garama za kutumia Bank Transfer kupitia SWIFT ni za juu kiasi, lakini ni njia inayokubalika. Kwa miamala ya kuanzia $10 hadi $700, unatozwa $15. Iwapo una zaidi ya $701, benki inatoza asilimia 1.5% ya jumla ya fedha unazotuma. Hii ina maana kwamba, kwa wengi, inakuwa vigumu kufikisha kiwango hicho cha $700, labda uwe umepanga kutoa pesa baada ya muda mrefu na kuongeza hadi ufikie kiwango hicho ndipo ufanye muamala wa benki.

Kwa hiyo, kuna njia nyingine ambayo wengi wanaiona ni bora zaidi na yenye unafuu, na nitakuelezea kwa undani hapa chini.

Njia Mbadala ya Kutoa Pesa Kutoka Payoneer

1. Kadi ya Virtual ya EUR

Njia hii imekuwa na unafuu kwa watu wengi. Unachotakiwa kufanya ni kuomba kadi ya virtual ya Euro (EUR) kupitia Payoneer. Baada ya hapo, unaweza kubadilisha fedha zako kutoka dola za Kimarekani (USD) kuwa Euro kwa gharama ya takribani 1.5%. Fedha hizi sasa zitakuwa kwenye kadi yako ya virtual.

Kisha, unachoweza kufanya ni kutumia kadi hii kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Binance kwa njia ya USDT (Tether). Baada ya hapo, tumia kipengele cha P2P kwenye Binance kuuza USDT zako moja kwa moja kwenda kwenye Mobile Money. Njia hii ina faida kwa sababu inaondoa hitaji la gharama kubwa za benki na inafanya muamala kuwa wa haraka zaidi.

2. Kutumia Paxful au Crypto Exchanges Zingine

Njia nyingine nzuri ni kutumia Paxful au crypto exchanges zingine zinazokubali muamala kupitia Payoneer. Katika hii, unachoweza kufanya ni kuweka ofa yako ya kupokea USD kutoka kwa mtu mwingine anayetumia Payoneer. Mara tu unapopokea fedha zako, utabadilisha kwa USDT na kuuza kwenda kwenye Mobile Money.

Hata hivyo, kuna kikwazo kidogo katika njia hii. Payoneer inahitaji akaunti yako iwe imeshapokea angalau USD 500 kabla hujaweza kufanya muamala na akaunti nyingine. Hii inamaanisha kwamba, ni lazima uwe tayari umeshafanya miamala kadhaa kabla ya kupata uhuru kamili wa kufanya malipo kwenda kwenye akaunti nyingine kwa urahisi.

Mapendekezo:

Kutoa Pesa Payoneer Kwenda Local Bank Inatumia Muda Gani?

Jinsi ya kutumia Payoneer

Ingawa NMB na CRDB zote ni chaguo linalowezekana kwa kutoa pesa kupitia Payoneer, ni muhimu kuzingatia garama za SWIFT na muda wa kusubiri. Njia mbadala za kutumia virtual cards na crypto exchanges kama Binance na Paxful zinaonekana kuwa na unafuu mkubwa zaidi, hasa kwa wale wanaotafuta njia za haraka na zenye gharama ndogo za kutoa pesa.

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.