Mafunzo ya JKT ni muda gani, Kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (National Service Act) ya mwaka 1964, wanafunzi waliohitimu kidato cha sita wanajiunga na JKT kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu (3).
Hii ni sehemu ya wajibu wao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Vijana hawa wanaoitwa “Vijana wa Mujibu wa Sheria” hufanya mafunzo ya kijeshi na maendeleo katika kambi mbalimbali za JKT.
Mafunzo ya JKT ni muda gani?
Baadhi ya maeneo ya mafunzo hayo ni:
- Ulinzi wa Taifa
- Uzalendo
- Ujasiliamali
- Ujasili (kupitia mafunzo ya Kilimo, Ufugaji na Biashara)
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea vijana nidhamu, uzalendo, ukakamavu na kuwapa ujuzi utakaowasaidia kuchangia katika ulinzi wa Taifa na maendeleo ya kiuchumi.
Baada ya kumaliza mafunzo ya miezi mitatu, vijana hawa huwa na fursa ya kuendelea na mafunzo ya kijeshi au kuajiriwa katika sekta mbalimbali za uchumi.
Kupitia JWTZ, inakubidi uwe umepigwa kwata la Kikuruta aka JKT kwa miezi sita.
Kisha baada ya hapo kama utabahatika kuchukuliwa JWTZ, itakubidi upige kozi kwa miezi mingine minne/mitatu. Kisha ndipo utaajiriwa rasmi. Kwa hiyo kama utanyooka moja kwa moja, inaweza kuchukua miezi 10 hadi 12.
Kwa muhtasari, muda wa mafunzo ya JKT kwa wanafunzi wa kidato cha sita ni miezi mitatu (3) kwa mujibu wa sheria. Mafunzo haya ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wa Tanzania kuwa raia bora na kuchangia katika maendeleo ya taifa.
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako