Majukumu Ya Mwandishi Msaidizi Wa Daftari La Kudumu La Wapiga Kura, Mwandishi Msaidizi ni mhimili muhimu katika mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Wajibu wao unahusu kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Baadhi ya majukumu yao muhimu ni:
Kuandikisha Wapiga Kura Wapya
- Kuandikisha wapiga kura wapya waliotimiza umri wa miaka 18 na zaidi
- Kuandikisha wale wote wenye sifa lakini hawakujiandikisha katika uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura awamu ya kwanza
Kuboresha Taarifa Za Wapiga Kura
- Kutoa kadi mpya kwa Wapiga Kura waliopoteza kadi zao
- Kuhamisha taarifa za Wapiga Kura waliohama Kata au Jimbo la Uchaguzi na kuhamia katika eneo jingine
- Kurekebisha taarifa zao Wapiga Kura ambazo zilikosewa
Kuondoa Wapiga Kura Wasio Na Sifa
- Kuondoa Wapiga Kura waliopoteza sifa kama vile kufariki
Kushirikiana Na Wadau Mbalimbali
- Kushirikiana na Mawakala wa Vyama vya Siasa katika vituo vya uandikishaji
- Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa
Kuzingatia Kanuni Na Taratibu
- Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya NEC
- Kuzingatia kanuni za afya na kufuata maelekezo utakayopewa kituoni, ili kuepuka maambukizi ya virusi
Mwandishi Msaidizi ana wajibu mkubwa katika kuhakikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaboresha kwa ufanisi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Ushirikiano wao na wadau mbalimbali pamoja na kuzingatia kanuni za afya ni muhimu katika kufikia lengo hili.
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako