Jinsi ya kulipia parking (Deni la parking na kulipia (TARURA))

Jinsi ya kulipia parking (Deni la parking na kulipia (TARURA)) Maegesho ya Magari, Kulipia deni la maegesho ya magari (parking) kupitia TARURA ni mchakato rahisi ambao unaweza kufanywa kwa kutumia simu yako ya mkononi kupitia mfumo wa malipo ya kielektroniki.

Hapa chini ni mwongozo wa jinsi ya kulipia deni la parking na TARURA (Termis) :

Jinsi ya Kulipia Deni la Parking TARURA

1. Kupitia USSD Code

  • Bonyeza *152*00# kwenye simu yako.
  • Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri).
  • Chagua namba 2 (TARURA).
  • Chagua namba 2 tena (Termis/angalia deni).
  • Ingiza namba ya usajiri wa chombo cha usafiri, kwa mfano, T544 AZZ.
  • Pokea ujumbe mfupi wenye deni lako na kumbukumbu namba ya malipo.

2. Kulipia Maegesho

  • Bonyeza *152*00# tena.
  • Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri).
  • Chagua namba 2 (TARURA).
  • Chagua namba 1 (Lipia Maegesho).
  • Ingiza kumbukumbu namba ya malipo na kisha thibitisha kiasi cha kulipa.

Malipo ya Parking TARURA

Hatua Maelezo
Kupitia USSD Code *152*00# kisha fuata maelekezo ya kuchagua TARURA na Termis
Kulipia Maegesho Ingiza kumbukumbu namba na thibitisha kiasi cha kulipa

Faida za Kulipia Deni la Parking TARURA

  • Urahisi wa Malipo: Mfumo wa USSD unarahisisha malipo bila haja ya kwenda ofisi za TARURA.
  • Kuepuka Adhabu: Kulipa kwa wakati kunasaidia kuepuka adhabu za kuchelewa kulipa.
  • Ufuatiliaji Rahisi: Unaweza kufuatilia malipo yako na deni kupitia simu yako.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kulipia deni la parking kupitia TARURA, unaweza kutembelea https://termis.tarura.go.tz/ kwa taarifa za ziada.

Nimebobea kwenye uandaaji wa makala za mtandaoni, Makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.