Mishahara ya Watumishi wa Umma 2024/2025, Katika mwaka wa fedha wa 2024/2025, serikali ya Tanzania imefanya mabadiliko makubwa katika viwango vya mishahara ya watumishi wa umma. Hii ni sehemu ya juhudi za kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi wa umma na kuongeza motisha katika utendaji kazi wao.
Mabadiliko haya yanahusisha nyongeza za mishahara na marekebisho katika ngazi mbalimbali za mishahara.
Viwango vya Mishahara kwa Walimu
Walimu ni miongoni mwa makundi ya watumishi wa umma ambao wamepata ongezeko la mishahara. Viwango vya mishahara kwa walimu vinavyotumika kuanzia mwaka 2024 ni kama ifuatavyo:
Ngazi ya Mshahara | Mshahara wa Mwanzo (Tshs.) | Nyongeza ya Mwaka (Tshs.) |
---|---|---|
TGTS B.1 | 479,000 | 10,000 |
TGTS B.2 | 489,000 | 10,000 |
TGTS B.3 | 499,000 | 10,000 |
TGTS C.1 | 590,000 | 13,000 |
TGTS C.2 | 603,000 | 13,000 |
TGTS D.1 | 771,000 | 17,000 |
TGTS E.1 | 990,000 | 19,000 |
Viwango vya Mishahara ya Watumishi wa Serikali
Serikali pia imeweka viwango vipya vya mishahara kwa watumishi wa serikali kwa mwaka 2024. Viwango hivi vinajumuisha nyongeza kwa watumishi katika ngazi tofauti za kazi:
Ngazi ya Mshahara | Mshahara kwa Mwezi (Tshs.) |
---|---|
TGS A.1 | 380,000 |
TGS B.1 | 450,000 |
TGS C.1 | 585,000 |
TGS H.1 | 2,110,000 |
Mabadiliko haya yanafuatia sera ya malipo ya mishahara na motisha katika utumishi wa umma, ambayo inahusisha ongezeko la asilimia 23.3 kwa kima cha chini cha mshahara.
Bajeti ya Ongezeko la Mishahara
Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 150.87 kwa ajili ya nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Tuachie Maoni Yako