Maombi Ya Vyuo Vya Afya 2024/2025 Tanzania, Ikiwa wewe ni mwanafunzi wa kidato cha nne au cha sita na unavutiwa na masomo ya diploma au cheti katika programu za Afya na Sayansi Mifugo, unahitaji kukamilisha maombi ya mtandaoni kwenye Mfumo wa Uhakikisho wa Kujiunga wa NACTE au kuomba moja kwa moja katika Taasisi ya Mafunzo.
Sifa za Kujiunga na Vyuo vya Afya
Ili kuwa na sifa ya kujiunga na programu za Afya na Sayansi Mifugo (HAS), mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa alama nne katika masomo yasiyo ya kidini katika mtihani wa kitaifa wa elimu ya sekondari (CSEE). Hata hivyo, kuna baadhi ya mahitaji maalum ya programu ambazo zinahitaji vigezo vya ziada.
Maelezo Muhimu ya Kujiunga
Ada za Vyuo vya Afya: Ada za vyuo vya afya hutofautiana kati ya vyuo vya umma na vya kibinafsi. Ni vyema kuangalia kwenye tovuti za vyuo husika kwa maelezo zaidi.
Mahitaji ya Kujiunga: Tazama taarifa za sifa za kujiunga na programu mbalimbali za afya kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Unaweza kupata mwongozo wa kujiunga kwa kubofya hapa au hapa.
Jinsi ya Kuomba
Kwa Vyuo vya Umma: Maombi yote ya vyuo vya umma yanafanyika kupitia mfumo wa maombi mtandaoni wa NACTE. Ni muhimu kujiandikisha mapema ili usikose nafasi.
- Tembelea tovuti rasmi ya NACTE https://www.nactvet.go.tz/ au hapa ili kujaza fomu za maombi mtandaoni.
- Fuata hatua zote zilizotolewa kwenye tovuti ili kukamilisha mchakato wa maombi.
Maombi ya vyuo vya afya ni fursa nzuri kwa vijana wanaotaka kujifunza na kujiandaa kwa kazi katika sekta ya afya. Hakikisha unafuata mchakato wa maombi kwa uangalifu na kuwasilisha maombi yako kwa wakati.
Mapendekezo:
Tuachie Maoni Yako