Vigezo vya ajira za Uhamiaji 2024, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, ametangaza nafasi za ajira mpya za Askari wa Uhamiaji kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa zifuatazo:
Sifa za Mwombaji
- Uraia:
- Mwombaji awe ni raia wa Tanzania.
- Mafunzo ya Jeshi:
- Awe amehudhuria na kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) au Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) waliopo Makambini au tayari amerudi uraiani.
- Ajira:
- Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini.
- Cheti cha Kuzaliwa:
- Awe na cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Taifa:
- Awe na kitambulisho cha taifa au nambari ya utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
- Afya:
- Awe na siha njema ya mwili na akili iliyothibishwa na daktari wa serikali.
- Dawa za Kulevya:
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
- Rekodi ya Uhalifu:
- Asiwe na kumbukumbu au taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai.
- Michoro Mwilini:
- Asiwe na alama yoyote au michoro (tattoo) katika mwili wake.
- Hali ya Ndoa na Watoto:
- Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto.
- Umri na Elimu:
- Mwombaji mwenye elimu ya kidato cha nne awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 23.
- Mwombaji mwenye elimu ya kidato cha sita na stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 26.
- Mwombaji mwenye elimu ya shahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.
- Utayari wa Kufanya Kazi:
- Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
- Gharama za Ufuatiliaji:
- Awe tayari kujigharimia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la ajira.
Kwa vijana wote wenye sifa zilizotajwa, mnakaribishwa kuomba nafasi hizi na kujiunga na Idara ya Uhamiaji ili kutoa huduma bora kwa taifa letu. Maombi yawe yamekamilika na kuzingatia vigezo vilivyotajwa ili kuepuka matatizo katika mchakato wa usaili.
Mapendekezo:
Nikitaka kJohnujisajili nafanyaje sasa