Kununua Tiketi za Mpira Vodacom M-Pesa

Jinsi Ya Kununua Tiketi za Mpira Vodacom M-Pesa, Kama unataka kununua tiketi za mpira bila kupitia usumbufu wa foleni ndefu, Vodacom M-Pesa ni suluhisho bora kwa ajili yako. Ukiwa na simu yako tu, unaweza kupata tiketi yako ndani ya dakika chache.

Huduma hii ni salama na inalinda taarifa zako za kifedha. Hapa chini ni mwongozo rahisi wa jinsi ya kununua tiketi za mpira kwa kutumia Vodacom M-Pesa.

Hatua za Kununua Tiketi za Mpira kwa Vodacom M-Pesa

  • Piga namba: *150*00#
  • Chagua namba 4: Lipa kwa M-Pesa
  • Chagua namba 9: Zaidi
  • Chagua namba 1: E-payment
  • Chagua namba 1: Tiketi za Michezo
  • Chagua namba 1: Tiketi za Mpira
  • Chagua mechi unayotaka kulipia
  • Chagua kiingilio unachotaka
  • Weka namba ya kadi ya N-Card
  • Ingiza namba yako ya siri
  • Thibitisha

Kwa kufuata hatua hizi rahisi, utaweza kupata tiketi yako ya mpira kwa haraka na bila usumbufu. Huduma hii ya M-Pesa inafanya maisha kuwa rahisi zaidi kwa mashabiki wa mpira. Furahia mechi zako bila wasiwasi wa kusimama kwenye foleni!

Soma Zaidi:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.