Tuzo za TFF Agosti 01, 2024 Award

Tuzo za TFF Agosti 01, 2024 Award, Hafla ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) – TFF Awards 2024 itafanyika Agosti Mosi, 2024 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki, Dar es Salaam.

Washindi na Vigezo vya Utoaji Tuzo

Washindi katika vipengele mbalimbali watatunukiwa tuzo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na TFF chini ya Kamati yake ya tuzo. Tunapenda kusisitiza kuwa katika vigezo hivyo, hakuna cha mashabiki kupigia kura walioteuliwa kuwania tuzo hizo (nominees). Hivyo, tunawaomba mashabiki na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla kupuuza kiunganishi (link) kinachosambazwa mitandaoni kuwataja wapige kura kuchagua washindi.

Onyo kwa Wanaosambaza Taarifa za Uongo

Pia tunawatakia wale wote wanaosambaza kiunganishi hicho kinachopotosha kuacha kufanya hivyo mara moja. Kuendelea kusambaza ni kutenda kosa.

Taarifa Rasmi kutoka TFF

Hii ni taarifa rasmi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na TFF Awards 2024. Tafadhali zingatia maelezo haya na epuka taarifa za upotoshaji. Kwa habari zaidi na taarifa sahihi, tembelea tovuti yetu rasmi au akaunti zetu za mitandao ya kijamii:

Tunaamini kuwa TFF Awards 2024 itakuwa hafla ya kukumbukwa ambapo tunatambua na kusherehekea mafanikio ya wachezaji wetu bora na wadau wa mpira wa miguu nchini Tanzania. Karibuni wote kushuhudia tukio hili la kihistoria.

Soma Zaidi:

Kazi Forums Ni chanzo chako bora cha makala na habari za kuaminika zilizochapishwa kwa weledi zaidi na uchunguzi wa kina.